Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNCDF kuimarisha maisha ya madereva lori Busia

UNCDF kuimarisha maisha ya madereva lori Busia

Nchini Uganda, serikali za mitaa zinashirikiana na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mitaji UNCDF ili kujenga kituo cha kuegesha malori mjini Busia, mpakani mwa Kenya.

Sasa hivi, madereva wanaoegesha malori yao mpakani wanakumbwa na hali ya wasiwasi wakikosa huduma za maji, malazi, chakula na utaratibu wa kupitia forodha ukichelewa zaidi.

Mradi huo wenye thamani ya dola milioni 2.5 unatarajiwa kuanza kutekelezwa mwisho wa mwaka huu kupitia ubia bunifu na sekta binafsi na hivyo kuimarisha usalama wa madereva na jamii nzima ya Busia.Lengo ni kujenga maegesho ya lami, pamoja na kuwapatia madereva huduma kama vile vyoo, hoteli, kituo cha mafuta, maduka na ulinzi. Ofisi za mamlaka ya ushuru ya Uganda zitajumuishwa pia.

Kulikoni? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hiyo.