Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

© Julius Mwelu/ UN-Habitat

Wagonjwa wasio na dalili kali za COVID-19 Kenya kutibiwa nyumbani

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 nchini Kenya ikifikia 300, serikali hii leo imetangaza mkakati wa kuepusha vituo vya afya na hospitali kuzidiwa uwezo wa kutibu wagonjwa hao.

Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus Oguna akizungumza jijini Nairobi, Kenya, amesema kuwa wagonjwa waliothibitishwa kuwa na virusi watatibiwa hospitalini, lakini wale wasio na dalili zozote za ugonjwa wataugulia makwao.

Sauti
2'40"

10 JUNE 2020

Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo:
-  Nchini Kenya Wagonjwa wasio na dalili kali za COVID-19 kutibiwa nyumbani
- Wakazi wa Mathare nchini Kenya washukuru UNICEF kwa kuwawekea tenki za maji
- UNICEF yachukua hatua kukabiliana na ukatili wa kingono Sierra Leone
-Na kwenya mashinani tunabisha hodi Nigeria kwa mwanariwanya mashuhuri Chimamanda Adichie Ngozi  nazungumzia jinsi ya kuondoa fikra potofu za wanaume juu a umiliki wa miili ya wanawake
-Na kwenye makala hii leo tuko katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kw
Sauti
13'42"