Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
COVID-19 kuporomosha uchumi wa nchi za Afrika kusini mwa Sahara kwa asilimia 1.6- IMF
Shirika la fedha duniani, IMF limetaja mambo matatu muhimu ya kuzingatiwa ili kuweza kupunguza madhara ya kibinadamu na kiuchumi yatokanayo na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.
Marekani amekuwa mshirika mkubwa wa WHO tunatumai ataendelea kuwa hivyo:Tedros
Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO amesema kwa muda mrefu Marekani imekuwa mshirika mkubwa wa WHO na anatimai kwamba itaendelea kuwa hivyo.
Uwepo wa COVID-19 unazua hatari kwa watoto muda waliopo mtandaoni
Mamilioni ya watoto wako hatarini kudhurika wakati huu ambao maisha yao yamehamia zaidi mitandaoni wakati wa kukaa ndani kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19, imeeleza taarifa iliyotolewa hii leo mjini New York Marekani na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF pamoja na wadau wake. Jason Nyakundi na maelezo zaidi
(Taarifa ya Jason Nyakundi)
Si wakati wa kupunguza rasilimali kwa shirika lolote lile la kibinadamu linalopambana na COVID-19-Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu si wakati wa kupunguza rasilimali za kufanikisha operesheni za shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO. Grace Kaneiya na ripoti kamili.
(Taarifa ya Grace Kaneiya)
Bwana Guterres amesema hayo katika taarifa iliyotolewa Jumanne usiku na msemaji wake jijini New York, Marekani akisema kuwa siyo tu kwa WHO bali pia si wakati wa kupunguza rasilimali kwa shirika lolote lile la kibinadamu linalopambana hivi sasa na ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19.
Watoto wako katika hatari zaidi ya kuathiriwa na muda mwingi mitandaoni wakati huu wa COVID-19-UNICEF
Mamilioni ya watoto wako hatarini kudhurika wakati huu ambao maisha yao yamehamia zaidi mitandaoni wakati wa kukaa ndani kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19, imeeleza taarifa iliyotolewa hii leo mjini New York Marekani na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF pamoja na wadau wake.
Uchumi wa dunia kuporomoka vibaya mwaka huu wa 2020-IMF
Mtazamo mpya uliotolewa na shirika la fedha duniani IMF kuhusu mwenendo wa uchumi duniani kwa mwaka huu 2020 unaonyesha kuwa ukuaji wa uchumi utakuwa katika hali hasi ya asilimia -3% kwa sababu ya mlipuko wa janga la virusi vya Corona au COVID-19.