Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani amekuwa mshirika mkubwa wa WHO tunatumai ataendelea kuwa hivyo:Tedros

Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus akitoa taarifa kuhusu mlipuko wa COVID-19 mjini Geneva
UN Photo/Eskinder Debebe)
Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus akitoa taarifa kuhusu mlipuko wa COVID-19 mjini Geneva

Marekani amekuwa mshirika mkubwa wa WHO tunatumai ataendelea kuwa hivyo:Tedros

Afya

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO amesema kwa muda mrefu Marekani imekuwa mshirika mkubwa wa WHO na anatimai kwamba itaendelea kuwa hivyo. 

Akizungumza na waandishi wa Habari hii leo kwa njia ya video mjini Geneva Uswis baada ya Rais wa Marekani kutangaza jana Jumanne kwamba inasitisha msaada kwa shirika hilo, Dkt. Tedros Adhamon Ghebreyesus amesema “Marekani imekuwa mshirika wa muda mrefu na rafiki mkarimu wa kwa WHO na tunatumai ataendelea kuwa hivyo. Tunasikitika kwa uamuzi wa rais wa Marekani kutoa amri ya kusitisha ufadhili kwa shirika la afya duniani. Kwa msaada wa wat una serikali ya Marekani, WHO inafanyakazi kuboresha afya ya watu wengi masikini na wasiojiweza duniani.”

Ameenda mbali zaidi na kusema WHO haipambani na virusi vya Corona au COVID-19 pekee, pia inafanya kazi kukabiliana na maradhi mengine kama polio, surau, malaria, Ebola, HIV, kifua kikuu au TB, utaiamlo, saratani, kisukari, afya ya akili na maradhi mengine mengi.

Pia inafanyakazi na nchi mbalimbali katika kuimarisha mifumo ya afya na kuboresha fursa za huduma za kuokoa maisha. 

Tumesikitika, tutajipanga

Dkt. Tedros ameoneza kuwa “WHO inatathimini athari za usitishaji wowote wa ufadhili wa Marekani katika kazi zetu na tutafanyakazi na washirika wetu kuziba pengo lolote la kifedha litakalotukabili na kuhakikisha kazi yetu inaendelea bila kuathirika. Jukumu letu kwa afya ya umma, sayansi na kuwahudumia watu wote wa dunia hii bila hofu wala upendeleo inasalia palepale. Lengo na wajibu wetu ni kufanyakazi na mataifa yote sawia, bila kujali ukubwa wa watu walionao au chumi zao.”

Na kwa mantiki hiyo ameweka bayana kwamba “COVID-19 haibagui baina ya na chi Tajiri na masikini, mataifa makubwa na madogo. Haibagui baina ya utaifa, makabila au Imani, nasi vivyo hivyo. Huu ni wakati wetu sote kushikamana dhidi ya changamoto hii ambayo ni tishiokubwa na adui hatari.”

Mgurugenzi huyo wa WHO amesema tunapogawanyika basi virusi hivyo vinatumia upenyo huo wa mgawanyiko wetu.

Tumejizatiti kuhudumia watu wa dunia hii na kuwajibika kwa rasilimali zote tunazopewa. Na kwa wakati muafaka kazi ya Who katika kukabiliana na mlipuko huu itatathiminiwa na nchi wanachama wa WHO na vyombo huru vilivyopo kuhakikisha uwazi na uwajibikaji. Hii ni sehemu ya mchakato wa kawaida uliowekwa nan chi wanachama . Na bila shama maeneo ya kuboreshwa yatabainishwa na kutakuwa na yale tya kujifunza kwetu sote. Lakini kwa sasa mtazamo wetu, mtazamo wangu ni kukomesha virusi hivi na kuokoa maisha.”

Tutaendelea kushirikiana na wadau

Ameongeza kuwa shirika hilo linaendelea kufanyakazi na wadau kote ulimwenguni ili kuchapuza utafiti na maendeleo ya dawa na chanjo za majaribio. 

“Zaidi ya nchi 90 zimejiunga ama zimeonyesha dharima ya kujiunga na mshikamano wa majaribio na zaidi ya wagonjwa 900 sasa wamesajiliwa , ili kutathimini usalama na utendaji wa aina nne za dawa na dawa mchanganyiko. Chanjo tatu tayari zimeanza majaribio, na zingine zaidi ya 70 ziko mbioni na tunashirikiana na wadau kusongesha kasi ya utengenezaji, uzalishaji na usambazaji wa chanjo.”

Na kuhusu hatua ambazo zinafanyika kuzisaidia nchi kupambana na janga hilo Dkt. Tedros amesema “jana ndege ya mshikamano ilianza safari ya kusafirisha vifaa vya kujikinga ,mashine za kusaidia kupumua na vifaa vya maabara kwa nchi nyingi barani Afrika. “

Ndege hiyo ya mshikamano ni sehemu ya juhudi kubwa za kusafirisha vifaa vya kitabibu kwa nchi 95 kote duniani kwa kushirikiana na shirika la mpango wa chakula duniani WFP, shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, fuko la kimataifa la ufadhili Global Fund, muungano wa chanjo duniani GAVI, Idara ya Umoja wa Mataifa ya operesheni za msaada msaada , UNITAID na wedau wengine.

Na mfuko wa mshikamano wa kupambana na janga la COVID-19 hivi sasa umekusanya takribani dola milioni 150 kutoka watu binafsi 240,000 na mashirika.

Tangu mwanzo wa mlipuko wa janga hili WHO imekuwa ikipamana nalo kwa kila hali na Dkt, Tedross ameahidi kwamba “tunaendelea kufanya hivyo hadi mwisho hiyo ni ahadi yetu kwa dunia nzima.”