Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Olle Mjengwa mshiriki wa Jukwaa la Vijana 2030, la Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC, akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano huo uliofanyika kwa siku tatu, New York ,Marekani.
UN/Assumpta Massoi

UNDP yashindanisha vijana kusaka majawabu kwa tabianchi , washindi kupata kitita cha fedha

Vijana wameelezwa kuwa na umuhimu mkubwa katika kusongesha mbele moja ya ajenda kubwa za 2030 za Umoja wa Mataifa ambayo ni kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi. Na katika kutambua mchango wao Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP, limekuja na mbinu mbalimbali za kuwashirikisha vijana ili wasiachwe nyuma katika suala hilo na mengine kama ya kuleta amani na usalama. Olle Mjengwa anayefanyakazi ya UNDP ofisi ya Roma Italia amezungumza na UN News kandoni mwa Jukwaa la vijana la Baraza la Kiuchumi na Kijamii ECOSOC lililokunja jamvi mwishoni mwa wiki ili kufafanua kuhusu ushirikishwaji huo wa vijana katika UNDP


 

Kamishina Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina Philippe Lazzarini
UN Photo/Evan Schneider

UNRWA iko tayari kutekeleza mapendekezo huru ya jopo la uchunguzi

Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA), Philippe Lazzarini, leo (23 Apr) aakizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani amerudia kusema anakaribisha mapendekezo ya ripoti iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kuhusu juhudi zake za kuhakikisha kutoegemea upande wowote na kujibu madai ya ukiukaji mkubwa yanapojitokeza.