DRC: Papa Francis ataka silaha ziwekwe chini, na wanaopora mali waondoke
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis aliyeko ziarani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amewasihi wakristo waweke silaha chini na badala yake wakumbatie huruma ya Mungu nchini humo. Radio Okapi ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO imesema Papa Francis amesema hayo leo wakati akihubiri kwenye misa iliyofanyika leo kwenye eneo la Ndolo, kitongoji cha Barumbu kwenye mji mkuu wa DRC, Kinshasa.