Watoto wangu wananiuliza Syria ni nini? Kambi ya Zaatar ikiingia muongo mwingine
Mwaka 2022 ni miaka 10 tangu kuanzishwa kwa kambi ya wakimbizi ya Za’atari nchini Jordan, kambi ambayo inasimamiwa na Umoja wa Mataifa. Ni kambi kubwa zaidi Mashariki ya Kati na moja ya kambi kubwa zaidi duniani ikiwa ni maskani ya wasyria 80,000. UN News au Habari za UN imezungumza na baadhi ya wakimbizi kuhusu maisha katika kambi hiyo, na matumaini yao kwa siku zijazo.