Somalia yaomba usaidizi kwa wahanga wa mafuriko
Rais wa Somalia Mohammed Abdullahi Mohammed Farmajoo amezuru maeneo yaliyokumbwa na mafuriko nchini humo hususuan maeneo ya kati ya nchi na kusihi jamii ya kimataifa isaidie wasomali 650,000 walioathiriwa na mafuriko hayo nchini kote.