Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mama anamsaidia binti yake mwenye umri wa miaka minane kuchukua masomo kwenye televisheni wakati wa janga la COVID-19 nyumbani Man, Côte d'Ivoire.
© UNICEF/Frank Dejongh

Umoja wa Mataifa na wadau wazindua kampeni ya #LetMeLearn kabla ya mkutano mkuu wa elimu 

Janga la elimu likichangiwa na janga la COVID-19, Umoja wa Mataifa unashirikiana na shirika la kutoa misaada kwa watoto la Theirworld na wadau wengine katika sekta hiyo, kuzindua kampeni ya #LetMeLearn au ‘Hebu nijifunze’, na kuwataka viongozi wa dunia kusikiliza sauti za vijana na kuweka mipango na fedha zinazohitajika ili kutoa elimu bora kwa kila mtoto. 

Tukio la kuwaaga walinda amani wa MONUSCO waliokufa wakati wa maandamano na uvamizi wa vituo vya ujumbe huo huko Goma na Butembo jimboni Kivu Kaskazini. (1 Julai 2022)
UN/Byobe Malenga

Walinda amani wa MONUSCO waliouawa katika maandamano DRC waagwa 

Viongozi wa Umoja wa mataifa pamoja na serikali ya Jamhuri ya Kidemoktrais ya Congo, DRC wametoa heshima zao za mwisho kwa walinda amani watano wa kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO waliokufa wakati wa maandamano na uvamizi wa vituo vya ujumbe huo huko Goma na Butembo jimboni Kivu Kaskazini. Walinda amani hao wanatoka Morocco na India ambapo Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Bintou Keita amesema MONUSCO iko tayari kwa mazungumzo ya amani ili kuendeleza na kudumisha amani nchini humo.

Sauti
2'29"
Mama akimnyonyesha mwanae hospitalini wadi ya kuzaliwa nchini India.
© UNICEF/Vinay Panjwani

Wiki ya unyonyeshaji: Usaidizi zaidi unahitajika kwa familia zilizopo katika mazingira hatarishi

Wiki ya Unyonyeshaji watoto maziwa ya mama duniani imeanza rasmi hii leo chini ya kauli mbiu yake isemayo Kuongeza Unyonyeshaji: Elimisha na Usaidizi, Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa serikali kutenga rasilimali zaidi ili kulinda, kukuza, na kusaidia sera na programu za unyonyeshaji, haswa kwa familia zilizo hatarini zaidi ambazo zinaishi katika mazingira ya dharura.

Sauti
2'33"