Mashirika ya UN yaomba kufunguliwe njia nyingine ya kufikisha misaada Gaza
Zikiwa ni zaidi ya siku 100 tangu kuibuka upya kwa mzozo huko Mashariki ya Kati, mashirika ya Umoja wa Mataifa hii leo yametoa taarifa inayoelezea kuongezeka kwa hatari ya baa la njaa na milipuko ya magonjwa ya kuambukiza huku yakisisitiza muarobaini pekee kwa sasa ni kuruhusu njia mpya za kuingiza misaada ya kwenda kutatua changamoto zinazowakabili wananchi walioko Gaza.