Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kauli za baadhi ya washindi wa Tuzo ya UN ya Haki za Binadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, (kati kulia mstari wa mbele) na Rais wa Baraza Kuu la UN Dennis Francis wakiwa na washindi wa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu mwaka 2023. Wa pili kulia mstari wa mbele ni Julienne Lusenge, Ra…
UN /Mark Garten
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, (kati kulia mstari wa mbele) na Rais wa Baraza Kuu la UN Dennis Francis wakiwa na washindi wa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu mwaka 2023. Wa pili kulia mstari wa mbele ni Julienne Lusenge, Rais wa SOFEPADI kutoka DRC.

Kauli za baadhi ya washindi wa Tuzo ya UN ya Haki za Binadamu

Haki za binadamu
  • Tuzo ikalete amani ya kweli mashariki mwa DRC - Lusenge
  • Tunachapisha kitabu kuelimisha haki ya mazingira safi- OFMCap
  • Tuzo imaanishe kutakuweko na mabadiliko kwenye changamoto

“Nimefurahi sana kupokea tuzo hii, na ni kwa ajili ya mashujaa wote walioweka rehani maisha yao kulinda maisha ya wengine nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,” amesema Julienne Lusenge, Rais wa shirika lisilo la kiserikali la mshimanano kwa ajili ya maendeleo ya wanawake SOFEPADI, nchini DRC.

Amesema kwa miaka 23 sasa shirika lao limekuwa mstari wa mbele kusaidia wanawake manusura wa ukatili wa kingono. Halikadhalika wanawake, wasichana na wavulana waathiriwa wa mzozo unaoendelea nchini mwao.

“Mapigano yamefanya kuwa vigumu watu kuishi nchini mwao. Tuna wakongo ambao ni wakimbizi wa ndani. Kila siku tunapambana kutetea haki, kupinga ukatili wa kingono. Shirika letu linapatia tiba, msaada wa kisaikolojia, tiba kwa manusura wa ukatili wa kingono. Lakini vile vile tunajengea uwezo wa kiuchumi manusura wa ukatili,” ameelezea Bi. Lusenge.

Tunasongesha haki kivitendo

Amefafanua kuwa shirika lao linatekeleza suala la kusongesha haki kivitendo kwa kupatia waathiriwa wa mapigano DRC misaada kama maji, vyakula, elimu kwa watoto na pia ulinzi wa haki na kurejesha amani.

“Bila amani hakuna haki,” amesema Lusenge akiongeza kuwa zaidi ya manusura 2,500 wa ukatili wa kingono wamepata matibabu SOFEPADI.

Amehitimisha hotuba yake akisema “kwa hakika niña furaha sana nikiwa na imani kuwa tuzo hii itamaanisha kutakuweko na umakini zaidi ili amani irejee nchini mwangu hususan eneo la mashariki ambako hakika hali ni tete.”

Harakati zimelipa sasa tunaenda kuchapisha kitabu cha haki

Baadhi ya wanachama wa Ushirikiano wa kimataifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Tuzo yao ya  Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu baada ya kuipokea jijini New York, Marekani 15 Desemba 2023.
OFMCap/Benedict Ayodi
Baadhi ya wanachama wa Ushirikiano wa kimataifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Tuzo yao ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu baada ya kuipokea jijini New York, Marekani 15 Desemba 2023.

Tuzo hii pamoja na kupatiwa mtu mmoja mmoja, hupatiwa pia makundi ambapo Ushirikiano wa kimataifa wa mashirika ya kijamii, watu wa asili, harakati za kijamii na jamii za mashinani umepata tuzo hiyo ikiwa ni mjumuiko wa mashirika mbali mbali.

Miongoni mwao ni shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la Wafransiskani wakapuchini ambapo Benedict Ayodi, mtawa kutoka shirika hilo amesema “shirika letu ni mojawapo ya mashirika yanayotuzwa kwa utetezi wao wa haki ya utetezi wa mazingira bora, mazingira safi na mazingira yenye uendelevu.”

Amesema wamefurahia sana kushinda tuzo hiyo, “sio sisi kama shirika, bali matokeo yake. Ni miaka mingi tumefanya utetezi wa haki hii, hivyo basi sisi kama wafransisko tunafuata mwongozo ya kwamba tunatetea wale wanyonge hasa wakati huu ambapo tunakumbwa na janga la tabianchi.”

Tweet URL

Ni wapi wafransiskani wanaendesha kazi zao?

Ayodi amesema, “baada ya hapa tutasukuma mataifa ili yaweze será kwenye nchi zao za kusaidia haki hiyo isongeshwe.”

Alipouliza nini walifanya hadi wakashinda tuzo, amesema “tulishirikiana zaidi ya mashirika 1350 duniani kote na kuwasilisha malalamiko ya watu wengi mbele ya Umoja wa Mataifa, huko Geneva, na New York, kuhusu madhara ya uchafuzi wa mazingira kwa afya zao.

“Kuna watu wanateseka kwa sababu ya pumu, hasa wale wanaoishi kwenye mazingira yenye viwanda vikubwa. Tunafurahi kuwa Umoja wa Mataifa umetusikiliza na kutambua haki hii.” Amesema Ayodi.

Ametolea mfano shughuli wanazofanya kama kule kwenye makazi ya mabanda huko Kibera na Mathare kwenye mji mkuu wa Kenya, Nairobi ambako amesema wafransisko wengi wanafanya kazi kuboresha mazingira ya maeneo hayo. Ametaja pia huko Brazili ambako uchimbaji madini unaharibu mazingira ya watu wa jamii ya asili, halikadhalika Papua New Guinea.

Nini kinafuata baada ya kushinda tuzo?

“Sasa tuna hii haki, na ni nyaraka, tunataka ifikie ngazi ya kitaifa, ili nchi ziweke kwenye será zao za kitaifa ili iweze kusaidia wananchi walioko mashinani,” amesema Ayodi.

Zaidi ya yote amesema wanaenda kuchapisha kitabu kuhusu haki ya mazingira. “Kitakueleza hii haki ya mazingira bora ina maana gani, na unaweza kuitumia namna gani hata kufanya utetezi wewe mwenyewe katika nchi yake, kwenda kwa wale aanasiasa na wale wawakilishi wetu ili waweze kuleta masuala haya na kuweka mazingira bora kwa watu wote.