Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DR Congo

Kundi la akina mama wa DRC wakionyesha idadi ya  watoto wao waliochukuliwa kwa nguvu kutoka majumbani mwao katika mkoa wa Tanganyika
UNHCR/Colin Delfosse

Hali itakuwa mbaya zaidi DRC bila misaada ya kibinadamu-Lowcock.

Bila msaada wa kibinadamu maisha ya raia wengi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yako mashakani. Onyo hilo limetolewa na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa anaehusika na masuala ya kuratibu misaada ya kibinadamu , Mark Lowcock wakati akilihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo na kuelezea hali ilivyo DRC.

Sauti
1'49"
Watoto wakimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa shirikala Umoja wa Mataifa la kukabiliana na UKIMWI, UNAIDS Michel Sidibé kabla ya mazungumzo yake na Mfale wa Bunyoro Dkt. Solomon Gafabusa Iguru wa II.
UNAIDS/Uganda

Heko Bunyoro kwa kupambana na UKIMWI-UNAIDS

Mfalme Iguru wa Pili, wa Bunyoro Kitara nchini Uganda  anasifika sana kwa kitendo chake cha kila wakati kutumia hotuba zake kuhamasisha watu wake kujikinga dhidi ya UKIMWI na hii imezaa matunda hadi kupatiwa pongezi na Umoja wa Mataifa.