Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wanaokimbia DRC, yavuka matarajio, Uganda: UNHCR

Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wakiwa katika kambi ya Kyangwali nchini Uganda. (Picha:© UNHCR/Isaac Kasamani)

Idadi ya wanaokimbia DRC, yavuka matarajio, Uganda: UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Kutoka Uganda shirika la Umoja wa Matifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasema mmiminiko wa wakimbizi kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasai ya Kongo (DRC), siku hizi umekuwa kinyume kabisa na matarajio , mwaka huu wakimbizi 60,000 wameingia, na kuibua changamoto katika utoaji wa misaada ya kibinadamu kwao. 

Joyce Munyao-Mbithi Afisa Mwandamizi wa Uhusiano wa UNHCR, Uganda ameniambia kwambia katika siku chahce zilizopita, wameanza kupokea wakimbizi Zaidi ya 1,000 kwa siku wakiwa wameangozeka kutoka wakimbizi kati ya 200 na 300 mapema wiki iliopita.

Amefichua kwamba wamepokea takriban elfu tano kabla ya kumaliza hata miezi mitatu ya mwaka huu ambamo walitarajia wakimbizi wasiozidi elfu sitini.

(SAUTI YA MUNYAO-MBITHI)

Munyao-mbithi ameongeza kuwa wanakabiliwa na changamto za kuwahudumia na kwmaba watakabiliwa na kipindi kigumu zadi endapo wahisani hawatajitolea kutoa misaada Zaidi.

(SAUTI YA MUNYAO-MBITHI)

Mgorgoro wa kikabila Jimboni Ituri na mashambulizi ya vikundi vilivyojihami katika Jimbo la Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ndio sababu ya mmiminiko huu wa wakimbizi

Munayo-mbithi amesema haya wakati UNHCR, na wadau wake wanakumbana na mlipuko wa maradhi ya kipindupindu amabyo kwa sasa yameambikia wakimbizi Zaidi ya 1,000 wakiwemo 33 waliothibitishwa kufariki dunia.

kuko nyuma zaidi na tatu kwa sababu ni wanawake hivyo fursa yao ya ICT iko nyuma sana”