Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Makala Maalum

Suala la kupoteza mtoto bado linachukuliwa kama mwiko au kitu cha aibu.
WHO/M. Purdie

Kwa nini tunahitaji kuzungumzia suala la kupoteza mtoto?

Kupoteza mtoto wakati wa ujauzito au ujauzito usio riziki bado ni jambo linaloonekana kama mwiko kulizungumzia ulimwenguni kote, mwiko unaoambatana na unyanyapaa na aibu. Wanawake wengi bado hawapati matunzo sahihi na ya heshima wanapopoteza ujauzito au kupoteza mtoto wakati wa kujifungua.