1 Novemba 2019

Kupoteza mtoto wakati wa ujauzito au ujauzito usio riziki bado ni jambo linaloonekana kama mwiko kulizungumzia ulimwenguni kote, mwiko unaoambatana na unyanyapaa na aibu. Wanawake wengi bado hawapati matunzo sahihi na ya heshima wanapopoteza ujauzito au kupoteza mtoto wakati wa kujifungua.

Mimba inapotoka au kuharibika ni dhahiri umpoteza mtoto wakati wa uja uzito. Lakini fikra huwa tofauti kutokana na sababu mbalimbali. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya ulimwenuni WHO asilimia 10  ya wanawake waliofamahu kuwa wao ni wajawazito hutambua mimba inapoharibika. Hali hiyo hufafanuliwa  na kupokelewa kwa  namna tofauti ulimwenguni, lakini kwa ujumla mtoto ambaye hufa kabla ya wiki 28  katika ujauzito huwa inasemekana kama upotezaji wa mimba, na watoto wanaokufa baada ya wiki 28 bado ni ujauzito usio riziki.

Kila mwaka, watoto milioni 2.6 hawaishi kutokana na mimba kuharibika au kutoka, na vifo vingi  kati ya hivyo vinaweza kuzuiliwa linasema shirika la afya duniani. Walakini, kupoteza mtoto au ujauzito usio riziki huwa hauwekei kumbukumbu kwenye mfumo wa usajili wa watoto , hata katika nchi zilizoendelea, na hivyo kudhihirisha kwamba idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi.

Ulimwenguni kote, katika nchi nyingi, hospitali na kliniki mara nyingi hazina rasilimali na waajiriwa wa kutosha. Unyanyapaa, aibu na hatia huwa ni suala la kawaida linalozungumzwa, wanawake ambao wamepoteza watoto wao hufanywa kuhisi kwamba wanapaswa kukaa kimya kuhusu huzuni yao, mara nyingi kwa sababu  kupoteza mimba na ujauzito usio riziki bado ni jambo linalochukuliwa kuwa ni la kawaida sana, au kwa sababu linaonekana kwamba haliwezi kuepukika.

WHO/M. Purdie
Suala la kupoteza mtoto bado linachukuliwa kama mwiko au kitu cha aibu.

Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara,  kwa kawaida inaaminika kwamba mtotomaliyekufa kabla ya kuzaliwa au kuharibika kwa mimba inatokana na masuala ya uchawi au mashetani.

Haya yote yanasababisha madhara makubwa kwa wanawake. Wengi wanaweza kukabiliana na masuala ya afya ya akili ambayo hudumu kwa miezi au miaka, hata wanapoendelea kuwa na watoto wengine wenye afya.

Larai, ni mfamasia aliye na miaka 44 kutoka Nigeria asimulia alipopoteza mtoto,

Kukabiliana na hali ya kupoteza ujauzito wa mtoto wangu iliniumiza sana. Wauguzi walichangia sana katika huzuni yangu licha ya mimi pia kuwa ni daktari. Suala lingine ni utamaduni. Katika tamaduni nyingi za Kiafrika, watu hufikiria kwamba unaweza kupoteza mtoto kwa sababu ya laana au uchawi. Hapa, upotezaji wa watoto huwa na unyanyapaa kwa sababu watu wengine wanaamini kuwa mwanamke anayepoteza mtoto mara kwa mara ana nuksi, au laana na pia inawezekana kuwa amekuwa mzinifu hapo awali na kwa hivyo upotezaji wake ujauzito ni kama adhabu kutoka kwa Mungu.”

WHO/M. Purdie

Watu, haswa wale walio na ushawishi mkubwa, wanazungumza kwenye mitandao ya kijamii kuhusu walivyokabiliana na masuala haya. Mmoja wao ni Kimberly Van Der Beek na mumewe, muigizaji James Van Der Beek, aliye na umaarufu sana katika fani ya filamu nchini Marekani ikiwemo iitwayo Dawson's Creek. Hivi karibuni walishiriki kwenye chapisho lililotolewa kwenye mtandao wa Instagram ambapo walizungumzia mchakato wa uchungu wa kupoteza ujauzito mara kadhaa, na kisha kujifunza jinsi walivyoweza kukabili hisia hizo na kuendelea na maisha.

"Nimepoteza ujauzito mara tatu, ukiwa na wiki 10. Nilikuwa na mume mwenye upendo, timu yenye huruma na nilihisi utulivu moyoni. Na hata katika hali nzuri, wote walinitia moyo. Lakini kinachonisikitisha ni kwamba sio wanawake wote, au baba ambaye pia anapata uchungu, wanaoshughulikiwa kwa huruma

au wanaoungwa mkono wakati huu mgumu wa masikitiko.

Unyanyapaa , huzuni na taharuki husababisha kutokuwepo kwa mazungumzo kuhusu kupoteza mtoto au ujauzito, na watu huhisi wapweke, kuchanganyikiwa, na mbaya ziadi, kulaumiwa”.

WHO/M. Purdie
Suala la kupoteza mtoto bado linatizamwa kama mwiko na kitu cha aibu.

Kupoteza mtoto kunaweza kusababishwa na hali isiyo ya kawaida ya mfuko wa uzazi, umri wa mama, maambukizo, ambayo mengi huzuilika kama vile ugonjwa wa malaria na kaswende, lakini sababu halisi ya maambukizi haya mara nyingi ni ngumu kuitatua.

Ushauri wa jumla wa kuzuia upoteaji wa watoto wakati wa ujauzito ni kama vile lishe bora, kufanya mazoezi, kujizuia kuvuta sigara, dawa za kulevya na pombe, kupunguza kiwango cha kafeini, kudhibiti mafadhaiko, na kuwa na uzito wa mwili unaofaa.

Hii inasisitiza mwenendo wa maisha, ambayo, kusipokuwa na sababu maalum kunaweza kusababisha wanawake kuhisi hatia kwamba wamesababisha kupoteza ujauzito wa watoto wao.

Kutana na Lisa, meneja masoko mwenye miaka 40, kutoka Uingereza. Lisa anasimulia alivyopoteza ujauzito mara kadhaa na jinsi ambavyo wahudumu wa afya hawahudumii haraka, wanawake waliopoteza watoto baada ya ujauzito kuharibika.

"Nimepoteza ujauzito mara nne kwa kipindi cha miaka nne. Kila ikitokea, unahisi ni kama nawe pia, umekufa kwa kiasi fulani. Kilichoniumiza sana ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuwa mjamzito. Tulipoenda hospitalini kuona mtoto anaendeleaje tumboni wakati wa kufanyiwa vipimo , niliambiwa kwamba mapigo ya moyo ya mtoto hayapo, ikimaanisha kuwa mtoto alikufa muda mrefu uliopita lakini mwili wangu haukuonyesha dalili zozote. Niliambiwa kuwa hata nilivyojua kuwa mtoto haukuwa hai, sera ya hospitali ilikuwa kwamba nisubiri wiki moja, halafu nirudi kupiga picha tena mimba ili kudhibitisha kuwa nimepoteza mtoto. Niliumia sana. Sikuweza kuamini kuwa narudi nyumbani nikiwa nimebeba mimba isiyo hai, na hakuna ushauri wowote juu ya nini cha kufanya”.

WHO/M. Purdie
Suala la kupoteza mtoto bado linachukuliwa kama mwiko au kitu cha aibu.

Kama ilivyo masuala mengine ya kiafya kama vile afya ya akili, ambayo bado kuna mwiko mkubwa kuijadili, wanawake wengi wanaripoti kuwa haijalishi tamaduni zao, elimu au malezi yao, marafiki na familia zao hawataki kuzungumzia jinsi walivyopoteza mtoto wakati wa ujauzito. Hii inatokana na ukimya wa kuzungumzia huzuni inayotokana na hali hiyo kwa ujumla.

Mtoto asiyeriziki hufanyika baadaye wakati wa ujauzito mtu 1 kati ya 2 hufanyika wakati wa uchungu wa kujifungua na, nyingi huweza kuzuilika. Takriban asilimia 98 ya ujauzito usio riziki hufanyika katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati limesema shirika la WHO.

Huduma bora wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua  kunaweza kuzuia ujauzito usio riziki kwa zaidi ya nusu milioni ulimwenguni kote. Hata katika nchi zenye kipato cha juu, utunzaji ni jambo muhimu kwa ujauzito usio riziki.

Kuboresha upatikanaji wa matunzo wakati wa ujauzito, kufuata muongozo unaotolewa na wakunga na kuelimisha jamii umuhimu wa matunzo wakati wa ujauzito inaweza kupunguza idadi ya watoto wanaokufa katika wakati wa ujauzito, ukijumuisha na matibabu ya maambukizo ya magonjwa mbalimbali wakati wa  ujauzito, vipimo vya mara kwa mara na uangalizi mkubwa wakati mama anapokuwa na uchungu wa kujifungua, vinaweza kuokoa watoto milioni 1.3 ambao wangezaliwa wamekufa au mimba kupotea.

UNFPA
Mwanasesere anayetumika kwa mafunzo na wakunga nchini Uganda.

Emilia, mfanyaniashara mwenye umri wa miaka 36 kutoka Colombia, anasimulia alivyopoteza mtoto wakati wa kujifungua  kutokana na huduma duni.

“Nilipokabiliwa na ujauzito usio riziki, mimba tayari ilikuwa ina wiki 32, na hata mtoto wangu tayari alikuwa na jina, aliitwa Julio Cesar. Nilikimbilia kliniki nikiwa na dalili za presha kupanda juu. Baada ya uchunguzi, daktari aliniambia nipumzike na akaniaandikia dawa ya kushusha presha, bila ushauri mwingine.

Baada ya wiki bado nilikuwa mgonjwa , kwa hivyo nilirudi kliniki. Daktari aliniharakisha kufanya uchunguzi na kisha akaniambia kuwa kuna jambo la kutatiza. Aliniambia kuwa mtoto haonyeshi dalili za uhai. Ninajua kuwa kupoteza mwanangu kungeweza kuepukwa, ikiwa tu ningepewa habari zaidi tangu mwanzo, na kupokea matibabu zaidi na sahihi wakati muhimu wa ujauzito wangu. Hakuna wakati wowote ambao nilipokea habari yoyote juu ya kile kilichotokea na Sikupokea ushauri wa aina yoyote.Nilijaribu kusaka majibu, nilifikiria mambo mabaya zaidi, ya kushangaza na kujilaumu, lakini nilijua kwamba haya hayakuwa sababu ya kumpoteza mtoto wangu”.

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud