Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Njia tatu za kuisaidia Afrika kupambana na Covid-19: UNECA
Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya kiuchumi kwa ajili ya Afrika UNECA, imeaninisha changamoto zinazolikabili bara la afrika katika hatua Madhubuti za kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19.
Dola trilioni 2.5 zahitajika kusaidia athari za COVID-19 za kijamii na kiuchumi kwa nchi zinazoendelea:UNCTAD:
Dola trilioni 2.5 zinahitajika ili kuzisaidia nchi zinazoendelea ambako theluthi mbili ya watu wote duniani wanaishi ili kuhimili athari za kijamii na kiuchumi kutokana na mgogoro wa virusi vya Corona, COVID-19.
COVID-19: Kijana Tanzania atengeneza ndoo ya kunawa mikono bila kugusa koki wala sabuni
Ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 ukiwa umeshasambaa katika mataifa 199 ikiwemo Tanzania, vijana nao wanaibuka na ubunifu mbalimbali ili kusaidia mataifa yao katika kudhibiti kuenea kwa gonjwa hilo lisilo na tiba wala chanjo. Ubunifu wa vifaa vya kudhibiti kuenea umefanywa na kijana mmoja nchini Tanzania kama anavyoripoti… wa kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam.
30 Machi 2020
Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.
JINGLE (04”)
ASSUMPTA:Ni Jumatatu ya Machi 30 mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI
Waajiri saidieni familia za wafanyakazi wakati huu wa COVID-19 – ILO/UNICEF
Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia watoto, UNICEF na lile la kazi, ILO leo wametoa mapendekezo ya jinsi waajiri wanaweza kusaidia waajiriwa na familia zao wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.
Janga la COVID-19 latishia kusambaratisha afya na uchumi katika nchi zinazoendelea:UNDP
Taarifa iliyotolewa leo na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP imeonya kwamba kusambaa kwa virusi vya Corona, COVID-19 kunatishia kusambaratisha nchi zinazoendelea sio katika mgogoro wa kiafya pekee wa muda mfupi bali janga la kijamii na kiuchumi kwa miezi na miaka ijayo.