Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola trilioni 2.5 zahitajika kusaidia athari za COVID-19 za kijamii na kiuchumi kwa nchi zinazoendelea:UNCTAD:

Nchi zinazoendelea kama Burkina Faso huenda zikahitaji msaada zaidi kutoka jumuiya ya kimataifa kutokana na athari za COVID-19
© UNICEF/Vincent Tremeau
Nchi zinazoendelea kama Burkina Faso huenda zikahitaji msaada zaidi kutoka jumuiya ya kimataifa kutokana na athari za COVID-19

Dola trilioni 2.5 zahitajika kusaidia athari za COVID-19 za kijamii na kiuchumi kwa nchi zinazoendelea:UNCTAD:

Ukuaji wa Kiuchumi

Dola trilioni 2.5 zinahitajika ili kuzisaidia nchi zinazoendelea ambako theluthi mbili ya watu wote duniani wanaishi ili kuhimili athari za kijamii na kiuchumi kutokana na mgogoro wa virusi vya Corona, COVID-19.

Hayo yameelezwa leo na taarifa ya tathimini iliyotolewa na kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo,UNCTAD.

Kwa mujibu wa kamati hiyo dola trilioni moja kati ya fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kupanua wigo kwa nchi kutumia kama akiba na malipo zikiwa zimetolewa na shirika la fedha duniani IMF.

Dola trilioni moja zingine ni kwa ajili ya madeni ya nchi zinazoendelea ambayo wataalam wa Umoja wa Mataifa ametaka yasamehewe kwa mwaka huu na bilioni 500 zitaenda kwenye mpango wa ufadhili utakaotolewa kwa nchi kufufua upya uchumi.

UNCTAD inasema athari za janga hili la Corona zinagusa kila kona na leo hii ni vigumu kusema na kutabiri nini kitakachotokea. “Matatizo ya kiuchumi yalyosababishwa na janga hili la corona yanakuwa kwa kasi yakipita kiwango kilichoshuhudiwa mwaka 2008. “

 Madhara ya janga hili la corona ynajidhihirisha na leo hii ni vigumu kutabiri nini kitakachotokea, lakini ni bayana kwamba hali katika nchi zinzoendelea itazorota zaidi kabla ya kuanza kuimarika tena-Mukhisa Kituyi.

Hali halisi kwa nchi zinazoendelea

Kwa mujibu wa tathimini ya UNCTAD kwa miezi miwili iliyopita wakati virusi vikisambaa nje ya China nchi zinazoendelea ziliathirika kutokana na kutokuweo na mtaji toka nje, mabadiliko katika mapato, kushuka kwa thamani ya sarafu za kitaifa, na kupungua kwa kipato ikiwemo mali ghafi na wimbi la watalii.

Na kutokana na hali ilivyo UNCTAD haitarajii kutengamaa haraka kama ilivyokuwa katika baadhi ya nchi baada ya mdororo wa kiuchumi wa mwaka 2008. Hivyo imesema kwa mwezi wa februari hadi Machi pato toka nje kwa nchi zinazoendelea lilikuwa dola bilioni 59 ukilinganisha na mwaka 2008 ambayo ilikuwa n idola bilioni 26.7.

Kwa upande wa bei za bidhaa ambazo ndio chacho cha pato kwa kusafirishwa nje kwa nchi zinzoendelea ilishuka kwa asilimia 37.

Hatua zinazochokululiwa

Waandishi wa ripoti hiyo ya tathimini wameeleza kwamba katika siku za karibuni nchi zinazoendelea na China zimechukua hatua za kufufua uchumi wao kwa kuwekeza dola trilioni 5.

Licha ya hatua hizo kwa mujibu wa wataalam nchi hizo zitakabiliwa na mdororo wa uchumi na hasara kubwa kwa mwaka huu. Kwa nchi nyingi zinazoendelea ukiacha China na India mdororo wa uchumi utawaathiri vibaya.

Juhudi za kufikia malengo ya maeneleo endelevu SDGs zitaathirika na kiwango cha maisha miongoni mwa watu kitashuka sana. Hata katika nchi zilizoendelea ajira zisizo rasmi ni changamoto na katika nchi zinazoendelea idadi kubwa ya watu wanapata kipato kutokana na njia hiyo nah ii inamaanisha kwamba wanakosa ulinzi wowote wa hifadhi ya jamii.Richard Kozul-Wright mkurugenzi wa UNCTAD anayehusika na masuala ya mkakati wa utandawazi na maendeleo amesema “Serikali za nchi zilizoendelea ziliahidi kufanya kila ziwezalo kusaidia raia wake, lakini zisikane wajibu wao wa kuonyesha mshikamano wa kimataifa na kuwalinda watu bilioni 6 wanaoishi kwenye nchi zilizo nje ya G-20.”

Mapendekezo ya UNCTAD

Hivyo wataalam wa UNCTAD wanapendekeza mkakati wenye vipengee vine ambavyo vinajumuisha kuwekeza fedha, kusamehe madeni, mpango wa kukufua uchumi na kudhibiti mitaji.

Kwa ujumla mpango huo uliopendekezwa unaenda sanjari na kiwango cha msaada ambao ungetolewa kwa nchi zinazoendelea katika miaka 10 iliyopita endapo nchi zilizojumuishwa kwenye kamati ya  msaada wa maendeleo ya shirika kwa ajili ya ushirikiano na maendeleo ingetimiza wajibu wake na kufikisha msaada wa maendeleo (ODA)ambao ni saw ana asilimia 0.7 ya pato la ndani la taifa GDP.