Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 Machi 2020

30 Machi 2020

Pakua

Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.

JINGLE (04”)      

ASSUMPTA:Ni Jumatatu ya Machi 30 mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI 

1: Waajiri saidieni familia za wafanyakazi wakati huu wa coronavirus">COVID-19 – ILO/UNICEF
Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia watoto, UNICEF na lile la kazi, ILO leo wametoa mapendekezo ya jinsi waajiri wanaweza kusaidia waajiriwa na familia zao wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. Flora Nducha na ripoti kamili.
(Taarifa ya Flora Nducha)
Taarifa yao ya pamoja iliyotolewa leo mjini New York, Marekani imesema kadri gonjwa hilo linavyozidi kusambaa, ni muhimu kusaidia familia kupunguza madhara yake kwa watoto wakisema kuwa, “kupoteza ajira, shule kufungwa na ukosefu wa huduma za malezi ya watoto kunamaanisha kwamba familia hasa zile zenye kipato cha chini zinahitaji msaada za ziada.”
 
Mkuu wa masuala ya uendelezaji watoto, UNICEF, Dkt. Pia Rebello Britto amesema kuwa, “Madhara ya COVID-19 ikiwemo kupoteza ajira, msongo wa kupitiliza na kudorora kwa afya ya akili kutagusa familia nyingi katika miaka ijayo. Kwa watoto wengi walio hatarini, ukosefu wa mifumo ya kutosha ya hifadhi ya jamii kunaongeza hatari ya wao kutumbukia zaidi kwenye madhara hayo.”
 
UNICEF na ILO wanatoa wito kwa serikali kuimarisha mifumo ya hifadhi ya jamii hususan kwa familia maskini ikiwemo kusaidia waajiriwa kuendelea na ajira na kupata kipato na kuwapatia hakikisho la usaidizi wa kifedha wale ambao wanapoteza ajira zao.
Mkurugenzi wa ILO kuhusu mazingira ya kazi Manuela Tomei anasema wao wanasisitizia mashauriano na ushirikiano baina ya serikali, wafanyakazi na waajiri pamoja na wawakilishi wa waajiriwa.
Mathalani, sera na vitendo ambavyo ni rafiki kwa familia kama vile ulinzi wa ajira za wafanyakazi na vipato vyao, likizo yenye malipo kwa ajili ya kuuguza au kutunza familia, saa za kazi ziendanazo na mahitaji ya mwajiriwa na kupata huduma bora ya malezi ya watoto.
Ni kwa kuzingatia msingi huo, mapendekezo ya mashirika hayo mawili ni pamoja na kufuatilia na kufuata ushauri wa mamlaka za kitaifa na kieneo na kusambaza taarifa hizo kwa wafanyakazi.
Pia kutathmni iwapo sera za sasa za pahala pa kazi zinatoa usaidizi wa kutosha kwa wafanyakazi na familia zao.

===================================================

2: COVID-19: Kijana Tanzania atengeneza ndoo ya kunawa mikono bila kugusa koki wala sabuni
 
Ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 ukiwa umeshasambaa katika mataifa 199 ikiwemo Tanzania ambako hivi sasa idadi ya wagonjwa imefikia 19, vijana nao wanaibuka na ubunifu mbalimbali ili kusaidia mataifa yao katika kudhibiti kuenea kwa gonjwa hilo lisilo na tiba wala chanjo. Ubunifu wa vifaa vya kudhibiti kuenea umefanywa na kijana mmoja nchini Tanzania kama anavyoripoti Ahimidiwe Olotu anayefanya mafunzo kwa vitendo katika kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam.
 
(Taarifa ya Ahimidiwe Olotu)
 
Jijini Dar es salaam nchini Tanzania katika moja ya karakana za uchomeleaji vyuma nakutana na kijana Joseph Sanga, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mbunifu wa ndoo ya kunawa mikono kwa maji na sabuni bila kushika koki wala sabuni.
 
(Sauti ya Joseph)
 
“Kwanza kabisa mashine hii, mfano wa kwanza nilifanya mwaka jana. Kwa maana ya kwamba nilijikita katika kuhakikisha kuwa tunanawa mikono bila kushika koki kwa sababu ya maambukizi ya magonjwa ya kuhara. Kwa hiyo niliangalia kwanza magonjwa ya kuhara, lakini baada ya kuja kwa gonjwa hili jipya baya nikaboresha ule mfano wa kwanza nikapta mashine hii ambayo yenyewe kwa kwa   sasa unanawa mikono kwa kukanyanga pedali na kisha unapata sabuni kwa kukanyaga pedali.
 
Pamoja na kusema kuwa kifaa hicho hakihitaij umeme na kinamudu mazingira magumu, Joseph akafafanua kinavyofanya kazi.
 
(Sauti ya Joseph)
 
“Hii ina pedali mbili, pedali ya kwanza ni kwa ajili ya sabuni na pedali ya pili ni kwa ajili ya maji.  Lakini kwenye pedali hii ya maji, kadri unavyoisukumu ndivyo kadiri unavyoongeza kiwango cha maji kutoka.”
 
Gharama kwa ndoo moja na sabuni na ndoo ya kukingia maji machafu ni shilingi 150,000, (Laki Moja na Nusu) ambapo Joseph anasema faida ni ndogo sana hivyo ana ombi..
 
(Sauti ya Joseph)
 
« Nikipata fursa ya kuonana na Waziri nitamuomba angalau anisaidie kwenye hili ili niweze kusambaza hivi vifaa kwa bei ya chini ,  nipate malighafi bila usumbufu, kodi pia niangaliwe ili nipate namna nzuri ili nisambaze vifaa zaidi na watu wengi zaidi wapate kunawa mikono. »
 
====================================================
STUDIO. MIDWAYSTING
====================================================
ASSUMPTA: 

Punde ni Makala na leo tuko Uganda kusikia hatua za kupambana na virusi vya Corona , COVID-19 vinavyoathiri wakimbizi. 
====================================================

3: Mradi wa wakimbizi kutengeza sabuni Za'atari unafanyika wakati muafaka:UNHCR

Kwa kutumia bidhaa za asili, wanawake wakimbizi kwenye kambi kubwa zaidi nchini Jordan wanatengeneza sabuni na kugawa kwa familia zilizo na mahitaji kwa ajili ya kusaidia katika kuzuia kuenea kwa virusi vya corona au COVID-19. Jason Nyakundi na taarifa zaidi

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)
 
Katika kambi ya wakimbizi ya  Za’atari tunakutana na wanawake wakiwa katika shughuli ya kutengeneza sabuni, kupitia video ya shirika la Umoja wa Msataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, hapa wanaonekana wakikatakata glycerin moja ya kiungo katika sabuni zao.

Wanawake hawa walipokea mafunzo kutoka Shirika la , UNHCR kama sehemu ya mradi wa Za’atari unaolenga kutoa mafunzo kwa wanawake. Um Mustafa, ni meneja, wa kikuundi cha Made in Za’atari ikimaanisha ilichotengenezwa Za’atari
 
 (Sauti ya Um)
“Sisi ni kundi la wanawake waliojifunza kuengeneza sabuni kwa ajili ya kusaidia familia zetu na sisi wenyewe.”
 
Wanawake hawa wanatumia viungo vya asili lakini pia kuna viungo vya ziada, kwenye video hii ya UNHCR wanaonekana wakimimina mchanganyiko wa rangi tofauti kwenye vyombo vya plastiki vyenye maumbo tofauti
(Sauti ya Um)
“Tunaongeza pia viungo tofauti kwa mfano rangi, marashi na na kileo kwa ajili ya kuifanya iwe bidhaa sio tu inayosafisha lakini pia inayotakasa mikono.”
Kwa upande wake Irene Omondi, meneja wa kambi hiyo ya Za’atari anasema
(Sauti ya Omondi)
“Ni mfano mzuri wa kutoa kwa jamii na kuzingatia usafi wakati kama huu kama UNHCR tunawajengea uwezo wanawake hawa na kuwapa mafunzo ya mradi wa Made in Za’atari kwa ajili ya kutengeneza vitu tofauti na kutumia stadi zao kutengeneza sabuni. Wanafanya kazi nzuri.”
Lengo la kutengeneza sabuni hizo ni lipi? Um anasema,
 
(Sauti ya Um)
“Tunatengeneza sabuni kwa ajili ya kusaidia wakimbizi wa Syria kwa sababu ni bidhaa muhimu.”

Programu hii sio tu inasaidia wanawake kuimarisha stadi zao lakini inahakikisha kwamba wakimbizi wanawaeza kunawa mikono yao kwa njia salama.
 
===================================================
STUDIO: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under
====================================================
ASSUMPTA:  Na sasa ni makala tuungane na mwandishi wetu wa Uganda John Kibego akizungumzaa na mkimbizi Access Bazibuha Mudosia kutoka DRC aliyeathirika na hatua za kupambana na virusi vya Corona Hoima.
=================================================
STUDIO: PLAY MAKALA
==================================================== 

ASSUMPTA: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under
====================================================
ASSUMPTA:  

Shukran sana mkimbizi Mudisia na John Kibego kwa makala hii
====================================================
Na sasa ni  mashinani ambapo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa Dokta Tedros Ghebreyesus anatoa wito kwa serikali kote duniani kuendeleza usitishaji wa shughuli za biashara ili kukabiliana na janga la virusi vya Corona.
====================================================
Studio: Play Mashinani
====================================================
ASSUMPTA: 
Asante sana  Dokta.Tedros Ghebreyesus kwa ujumbe huo.
==================================================
STUDIO: Play Bridge

ASSUMPTA: Na hadi hapo natamatisha jarida letu la leo. Tupatane kesho kwa habari na makala kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa unaweza kupata matangazo na taarifa nyingine na kujifunza Kiswahili kwenye wavuti wetu news.un.org/sw. Msimamizi  wa matangazo ni FLORA NDUCHA na fundi mitambo na mimi ASSUMPTA MASSOI, nasema kwaheri kutoka New York. 

==================================================
TAPE: CLOSING BAND

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
11'22"