Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Cindy McCain akiwa ziarani huko Laos mnamo Novemba 2022 kabla ya kuthibitishwa kwake kama Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo.
© WFP/Lee Sipaseuth

Cindy McCain ashika rasmi hatamu WFP wakati uhakika wa chakula duniani ukiwa njiapanda

Cindy H. McCain leo Jumatano amejiunga rasmi na shirika la Umoja wa Mataifa la cpango wa chakula duniani WFP, kama mkurugenzi mtendaji wake mpya, akionya kwamba dunia inakabiliwa na janga la chakula ambalo halijawahi kushuhudiwa ambalo linalitaka shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Roma Italia kukusanya rasilimali zaidi kwa haraka, kuwa bunifu zaidi na kuendeleza ushirikiano mpya wenye malengo makubwa kwa ajili ya mustakbali wa chakula duniani.