Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Jeannette Niyibigira, mshoni na mnufaika wa mkopo unaofadhiliwa na UNICEF na shirika la kiraia la Foi en Action akisalimia wakazi wenzake wa kambi ya wakimbizi wa ndani ya Gatumba karibu na mji wa Bujumbura nchini Burundi.
© UNICEF/Karel Prinsloo

Kama si UNICEF na mdau wake Foi En Action, nisingefika popote - Jeannette Niyibigira 

Kutokana na mabadiliko ya mifumo ya mvua, hali ambayo imekuwa ikileta maafa nchini Burundi na kusababisha mafuriko, maporomoko ya ardhi na kuharibu mazao, Jeannette Niyibigira, pamoja na mumewe na watoto 5, walilazimika kuyahama makazi yao ya Gatumba, na sasa wanaishi katika kambi ya Kiragaramango ambako kama si mkopo mdogo kutoka shirika la Foi En Action (Faith in Action) ambalo ni wadau wa UNICEF, Camp, maisha yangekuwa magumu zaidi.