Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

02 FEBRUARI 2023

02 FEBRUARI 2023

Pakua

Hii leo katika Jarida tunakuletea Habari kwa Ufupi, Mada kwa Kina na Jifunze lugha ya Kiswahili.

Katika Habari kwa Ufupi Leah Mushi anamulika ziara ya Papa Francis nchini DR Congo na wito wake kwa vijana na viongozi wa dini kukataa rushwa. Halikadhalika anamulika maeneo oevu na umuhimu wake bila kusahau nchini Sudan Kusini ambako Umoja wa Mataifa unaendelea kutoa misaada kwa familia zilizokimbia kutoka katika eneo la Pibor.

Mada kwa Kina inamulika mmea aina ya Azolla, hili ni gugu maji na ni kwa vipi nchini Tanzania limeanza kuchangamkiwa na vijana katika kujiongezea kipato.

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ni msemo ya kwamba sikio halilali njaa.

Karibu na mwenyeji wako ni Anold Kayanda.

Audio Credit
ANOLD KAYANDA
Audio Duration
12'