Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 FEBRUARI 2024

23 FEBRUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini DR Congo na hali ya msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi wake. Pia tunakupeleka nchini Burundi kufuatilia kazi za makundi ya kijamii. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Ukraine tukielekea miaka mwili kamili ya vita nchini humo.

  1. Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP leo yametoa wito wa kuchukuliwa hatua mara moja kuwalinda watoto na familia zao waliojikuta katikati ya machafuko yanayoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, huku lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR likielezea wasiwasi mkubwa kuhusu mustakabali wa zaidi ya raia milioni 7 waliotawanywa na kuomba msaada zaidi kutoka jumuiya ya kimataifa.
  2. Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP Kanda ya Afrika, Ahunna Eziakonwa yuko ziarani nchini Burundi ambako amekutana na makundi mbalimbali ya kijamii na hata kufika mpaka wa Burundi na DRC kuona uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo. 
  3. Makala inatupeleka katika chuo kikuu cha Nairobi Kenya ulikomalizika mkutano wa wanawake katika nyanja ya diplomasia. Huko viongozi wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Nairobi na Geneva Uswisi wamewasilisha mada mbele ya umati wa watu wakiwemo Mabalozi wastaafu na wa sasa wanaowakilisha mataifa yao Kenya kuhusu nafasi ya mwanamke katika diplomasia na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Dkt. Elizabeth Kimani Murage anayefanyakazi na kituo cha utafiti na idadi ya watu Afrika kama mtafiti mkuu, ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo.
  4. Katika mashinani tukielekea miaka mwili kamili ya vita nchini Ukraine tutamsikia mmoja wa waathirika wa vita hiyo.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
10'53"