Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA, Mark Lowcock leo ametangaza kwamba mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umetenga dola milioni 3 kama mchango wa kuwasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko ya ardhi na maporomoko ya udongo nchini Kenya.
Mahitaji ya kibinadamu nchini Sudan ni makubwa na yanachangiwa na sababu mbalimbali amesema mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA.
Wakimbizi wa Syria zaidi ya 12,000 wamesaka hifadhi katika nchi jirani ya Iraq tangu kuzuka wimbi kubwa la wakimbizi siku nne zilizopita kwa mujibu wa timu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.
Watoto takriban 490,000 wameathirika na mafuriko makubwa nchini Sudan Kusini limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF na kuongeza kuwa mvua kubwa zilizoanza kunyesha tangu mwezi Julai mwaka huu zimeathiri jumla ya watu 908,000 katika kaunti 32.
Licha ya hatua kiasi zilizopigwa nchini Syria hususan baada ya mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kufanya ziara , lakini hali bado ni tete katika baadhi ya maeneo ikiwemo Idlib amesema msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kibinadamu na naibu mratibu wa misaada ya dharura Ursula Muller akitoa tarifa katika Baraza la Usalama hii leo jijini New york Marekani.
Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Denise Brown amesema mapigano katika mji wa kasakzini Mashariki mwa nchi hiyo wa Birao, jimbo la Vakaga ,yamesababisha janga kwa wakazi na ni ukiukaji wa haki za binadamu.
Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Denise Brown amesema mapigano katika mji wa kasakzini Mashariki mwa nchi hiyo wa Birao, jimbo la Vakaga ,yamesababisha janga kwa wakazi na ni ukiukaji wa haki za binadamu.
Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema limetiwa moyo na tarifa za ufadhili mpya kwa ajili ya Yemen ingawa bado taifa hilo linakabiliwa na pengo kubwa la fedha kwa ajili ya huduma za kibinadamu.
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Martin Griffiths amesema anatiwa hofu kubwa kuhusu mashambulio yaliyofanywa na ndege isiyo na rubani au drine katika vituo viwili vya mafuta kwenye Ufalme wa Saudi Arabia.