Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

17 MACHI 2023

17 MACHI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea habari za WHO nchini Burundi na UNICEF eneo la Sahel. Makala tutamsikia mwanafunzi kutoka Tanzania ambaye ni mshiriki wa mkutano wa  67 wa  Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW67 na mashinani tutasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe kuhusu haki ya maji.

  1. Mamlaka ya afya nchini Burundi leo imetangaza mlipuko na kusambaa kwa virusi vya polio type 2 baada ya wagonjwa wanane kuthibitishwa , ikiwa ni mara ya kwanza kuthibitishwa kwa virusi hivyo baada ya zaidi ya miongo 3 kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO.
  2. Watoto milioni 10 nchini Burkina Faso, Mali na Niger wana uhitaji mkubwa wa misaada ya kibinadamu, idadi ambayo ni maradufu ikilinganishwa na mwaka 2020, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto duniani, UNICEF hii leo, chanzo kikiwa ni mizozo inayoshamiri kila uchao na kwamba Watoto wengine million 4 nchi Jirani wako hatarini Zaidi kwani mapigano kati ya makundi yaliyojihami na majeshi ya serikali yanavuka mipaka.
  3. Katika Makala mwanafunzi kutoka Tanzania ambaye ni mshiriki wa mkutano wa  67 wa  Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW67 unaomalizika leo, amezungumza na Selina Jerobon wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa mataifa kuhusu kilichomleta kwenye mkutano huu na matarajio yake katika ulimwengu huu wa kidijitali.
  4. Na katika mashinani ikimulika ujumbe kuhusu haki ya maji ikiwa ni kuelekea mkutano wa Umoja wa Mataifa wa maji utakaofanyika wiki ijayo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
14'5"