Burkina Faso

Hali tete wakimbizi wa ndani nchini Burkina Faso

Dharura kubwa ya kibinadamu inajitokeza nchini Burkina Faso ambapo kuongezeka kwa ukosefu wa usalama na mizozo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kumesababisha mzozo unaokua kwa kasi zaidi wa makazi, watu zaidi ya milioni wakifurushwa kutoka katika makazi yao. Taarifa ya Ahimidiwe Olotu, i

Sauti -
3'19"

16 Februari 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha aanza na ombi la dola milioni 222 kwa ajili ya wakimbizi wa Burundi waliosaka hifadhi nchi jirani za Tanzania, DRC na Rwanda.

Sauti -
13'12"

Naibu Mkuu wa OCHA atembelea Burkina Faso, ashuhudia hali ilivyo tete

Dharura kubwa ya kibinadamu inajitokeza nchini Burkina Faso ambapo kuongezeka kwa ukosefu wa usalama na mizozo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kumesababisha mzozo unaokua kwa kasi zaidi wa makazi, watu zaidi ya milioni wakifurushwa kutoka katika makazi yao.

Ukisikia kuruka maji kukanyaga moto ndio kiwakutacho wakimbizi kutoka Burkina Faso

Nchini Burkina Faso, watu waliofurushwa katika makazi yao, wanahangaika kutafuta kimbilio dhidi ya vurugu na athari za mabadiliko ya tabianchi. Baada ya kuacha nyumba zao, ambako ukame umekuwa wa kawaida, maelfu ya watu wakati huo huo wanakabiliwa na mafuriko makali ambayo yalifuta makazi yao.

Sauti -
1'58"

26 Januari 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanzia Msumbiji ambako kimbunga Eloise kimetonesha kidonda cha manusura wa vimbunga Chalane na Idai. Kisha atabisha hodi Burkina Faso akimulika raia waliokimbia vurugu makwao wakikumbwa na janga la mabadiliko ya tabianchi.

Sauti -
13'6"

Raia wa Burkina Faso wanazikimbia vurugu, wanapokelewa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi

Nchini Burkina Faso, watu waliofurushwa katika makazi yao, wanahangaika kutafuta kimbilio dhidi ya vurugu na athari za mabadiliko ya tabianchi. Baada ya kuacha nyumba zao, ambako ukame umekuwa wa kawaida, maelfu ya watu wakati huo huo wanakabiliwa na mafuriko makali ambayo yalifuta makazi yao.

Hatua mpya za usalama zaruhusu wakimbizi wa Mali kurejea kambini kutoka Burkina Faso

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limewasaidia wakimbizi 3,000 kutoka Mali kurejea kambi ya Goudoubo nchini Burkina Faso miezi tisa baada ya ukosefu wa usalama kuwalazimisha kuhama.
 

Heko Burkina Faso kwa kuweka mazingira bora ya mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu Kesho:Guterres

Katika mkesha wa kuamkia uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge nchini Burkina Faso hapo kesho Jumapili Novemba 22, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameipongeza serikali, viongozi wa kisiasa na watu wa Burkina Faso kwa kudumisha mazingira ya kuheshimiana katika wakati wote wa mchakato wa uchaguzi licha ya changamoto lukuki zinazolikabili taifa hilo la Afrika Magharibi.

Hatua za haraka zahitajika kuepusha baa la njaa katika nchi nne:WFP/FAO  

Mamilioni ya watu katika nchi nne zilizoghubikwa na tatizo la kutokuwa na uhakika wa chakula za Burkina Faso, Kaskazini mwa Nigeria, Sudan Kusini na Yemen wanahitaji msaada wa ili kuepuka kutumbukia katika baa kubwa la njaa yameonya leo mashirika Umoja wa Mataifa ya misaada ya kibinadamu. 

UNHCR imelaani vikali mauaji ya wakimbizi wa ndani 25 Burkina Faso 

 Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limelaani vikali shambulio ambalo limekatili maisha ya wakimbizi wa ndani 25 nchini Burkina Faso.