14 APRILI 2020
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Maaifa hii leo Flora Nducha anakuletea
-Uganda yaongeza muda wa wiki tatu kutekeleza sheria za kupambana na virusi vya Corona au COVIDI-19 ikiwemo marufuku ya kutembea usiku, kutumia usafiri wa umma na magari binafsi.
-Watoto milioni 117 kote duniano wako katika hatari ya kukosa chanjo ya surua ya kuokoa maisha kutokana na mlipuko wa COVIDI-19 yameonya mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNICEF na WHO
-Mkurugenzi wa shirika la afya duniani WHO kanfa ya Afrika Dkt. Matshidiso Moeti amesema ilichojifunza afrika kutokana na Ebola chaweza kusaidia katika vita dhidi ya COVID-19
-Makala leo inatupeleka visiwani zanzima kuangazia mafunzo ya chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA yalivyosaidia kulinda afya na mama na mtoto
-Na mashinani tunabisha hodi Kenya kwa manakandanda wa timu ya taifa ya nchi hiyo Harambee stars akitoa wito kwa umma kujilinda na virusi vya Corona.