15 Julai 2019

15 Julai 2019

Miongoni mwa yale anayokuletea assumpta Massoi katika Jarida letu la Habari leo ni pamoja na 

-Kisa kipya cha Ebola chaibuka Goma DRC , shirika la afya WHO na serikali wanafanya kila njia kuzuia kusambaa kwa mlipuko huo

- Watoto milioni 20 hawakupata chanjo muhimu ya kuokoa maisha 2018 yasema mashirika ya UNICEF na WHO na kutaka kila nchi kuchukua hatua kuhakikisha watoto wote wanachanjwa

-Onyo limetolewa na shirika la afya duniani WHO kuwa vyakula vya watoto wachanga wa chini ya umri wa miezi sita vimejaa sukari

-Makala yetu leo inamulika uhifadhi wa mazingira ya bahari visiwani Zanzibar

-Na mashinani tuko Canada kwake Zipporah Ogot akiwaasa hususani wasichana kwamba elimu haichagui umri na haina kuchelewa

Audio Credit:
UN News/assumpta Massoi
Audio Duration:
12'15"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud