Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makaburi ya wayahudi mjini Fez nchini Morocco, ushahidi wa jamii tofauti kuishi pamoja kwa amani

Makaburi ya wayahudi mjini Fez nchini Morocco, ushahidi wa jamii tofauti kuishi pamoja kwa amani

Pakua

Umoja wa Mataifa unasema robo tatu ya migogoro mikuu ya ulimwengu ina uhusiano na masuala ya kitamaduni na kwa hivyo kuziba pengo kati ya tamaduni ni jambo la haraka na la lazima kwa ajili ya amani, utulivu na maendeleo. Makaburi ya Kiyahudi huko Fez, Morocco ni ushuhuda wa utamaduni tofauti kuishi pamoja kwa amani.

Wakiwa katika safari ya kikazi huko Fez, kuangazia Mkutano wa tisa wa Jukwaa la Umoja wa Mataifa la Muungano wa Ustaarabu, UNAOC, May Yacoub na Alban Mendes De Leon kutoka Timu ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa walikutana na Johanna Devico Ohana, mzaliwa wa Fez, ambaye anatunza makaburi haya yenye umri wa miaka 200, akiheshimu jina la marehemu babake ambaye mwenyewe alikuwa msimamizi wa utunzaji wa makabuli haya hadi  alipoaga dunia miezi michache iliyopita. Anold Kayanda anasimulia makala hii kwa lugha ya Kiswahili.

Audio Credit
Selina Jerobon/Anold Kayanda
Audio Duration
3'51"
Photo Credit
UN News