Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiwanda cha tiba lishe ni mkombozi kwa watoto wenye unyafuzi Pembe ya Afrika

Kiwanda cha tiba lishe ni mkombozi kwa watoto wenye unyafuzi Pembe ya Afrika

Pakua

Nchini Kenya, mfululizo wa misimu mitano bila mvua umeathiri maisha ya jamii zilizo hatarini. Vyanzo vya maji vimekuwa mbali, mimea imekauka, mifugo nayo imekufa. Mambo yote haya yamesababisha watu kutokuwa na uhakika wa kupata chakula, halikadhalika kupungua kwa uzalishaji wa maziwa, bei za vyakula zimepanda, bei za nishati huku uwezo wa watu kununua bidhaa umeporomoka.

Watoto nao hali zao za lishe zimezidi kudorora ambapo hadi mwezi Juni mwaka 2022 kitaifa asilimia 26 ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini Kenya, au tuseme watoto milioni 1.5,  walikuwa na utapiamlo mkali au unyafuzi. Sekta binafsi kwa ushirika na Umoja wa Mataifa imechukua hatua kuhakikisha watoto hao wanapona unyafuzi na miongoni mwao ni kiwanda cha Insta kinachozalisha chakula lishe ambacho ki tayari kuliwa na mtoto na kina virutubisho au kwa kifupi kiingereza RUTF. Makala hii inakuletea kwa kina kuhusu kiwanda hicho na kauli ya UNICEF. Msimulizi wako ni Thelma Mwadzaya. 

Audio Credit
Thelma Mwadzaya
Audio Duration
4'58"
Photo Credit
© UNICEF/James Ekwam