Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu ya usuluhishi na haki kusaidia kufanikisha SDGs Morogoro, Tanzania

Elimu ya usuluhishi na haki kusaidia kufanikisha SDGs Morogoro, Tanzania

Pakua

Lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu SDGs yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015 linasisitiza amani, haki na taasisi thabiti. Uvunjivu wa amani utokanao na migogoro kwenye jamii ni moja ya maeneo yanayomuikwa ili kuhakikisha amani inakuweko na hivyo kuwezesha kufikia SDGs mwaka 2030.

Nchini Tanzania, wiki ya sheria imefungua pazia na Mahakama Kuu inatimiza wajibu wake kusaidia nchi kufanikisha SDGs. Mathalani mkoani Morogoro, Mashariki mwa taifa hilo, Mahakama Kuu imesema sasa itasongesha zaidi elimu ya usuluhishi na haki kwa lengo la sio tu kujenga amani bali pia kuchochea uchumi. Je nini kinafanyika? Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM alikuwa shuhuda wetu na ameandaa makala hii, 

Audio Credit
Selina Jerobon/Hamad Rashid
Audio Duration
4'21"
Photo Credit
UN News