Baba yangu asingemruhusu mama kusoma, nani angalikuwa anamlea hivi sasa? - Getrude
Suala la usawa wa jinsia ni suala mtambuka ambalo linahusisha taasisi mbalimbali ili liweze kufanikiwa katika taifa lolote lile. Hata hivyo taasisi ya familia ndio msingi mkuu wa kujenga au kubomoa dhana hii ambayo ni muhimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Nchini Tanzania, msichana Getrude ni shuhuda wa jinsi familia yake imekuwa msingi imara wa kutekeleza kwa vitendo usawa wa jinsia na sasa ameona matunda na kuamua kutumia uzoefu wake kunusuru watoto wa kike na wasichana ili wasitumbukie kwenye mtego wa kuwaengua na manufaa ya usawa wa jinsia. Je ni kwa vipi?