Viongozi wakifahamu kuhusu mabadiliko ya tabianchi, kazi inakuwa rahisi: UNEP

17 Disemba 2018

Mkutano wa 24 wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (COP24) umekamilika huko mjini Katowice Poland. Baada ya wiki mbili za majadiliano ya makundi zaidi ya 200 yameidhinisha muongozo wa utekelezaji wa mkataba wa Paris wa mwaka 2015, wenye lengo lakupunugza ongezeko la joto duniani kuwa chini ya nyuzi joto 2.

Mkutano huo umeeleza kuwa ingawa kuna hatua ambazo zimepigwa, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kufikia makubaliano ya mkataba wa Paris hasa kwa nchi zinazoendelea.

Ni changamoto gani ambazo zinasababisha nchi zinazoendelea, hasa za kiafrika kushindwa kufikia makubaliano ya Paris. Stanford Mwakasonda, afisa kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP anayehusika na kitengo cha kuzisaidia nchi zinazoendelea akihojiwa na Yasmina Guerda wa UN news kandoni mwa mkutano huo anaeleza katika makala hii iliyosimuliwa na Assumpta Massoi…

Audio Credit:
Assumpta Massoi/ Stanford Mwakasonda
Audio Duration:
2'41"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud