Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

UNIS/Stella Vuzo

Mlo shuleni umeongeza idadi ya wanafunzi wangu shule ya Salama: Mwalimu Beatrice Nyakoa Osaka

Shule ya Salama iliyo katika eneo la Huruma karibu na mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi Kenya hivi karibuni imeanza programu ya mlo shuleni kupitia mradi wa kampuni ya ‘Food for Education”. Hatua hiyo imenfa idadi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo kuongezeka kutoka 1, 900 hadi 2,300. Mlo shuleni ni moja ya masuala ambayo yanapigiwa debe kubwa na Umoja wa Mataifa sio tu kwa sababu ya kuhakikisha lishe bora kwa mamia ya maelfu ya wanafunzi ambao wengi hawawezi kupata mlo nyumbani bali pia kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria masomo.

Sauti
6'7"
UN News/Stella Vuzo

Mkutano wa UNEA 6umekuwa fursa kubwa kwangu – Mfugaji kutoka Tanzania

Mkutano wa 6 WA Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 umefunga pazia leo jijini Nairobi, Kenya baada ya siku 5 za majadiliano na shughuli mbalimbali zilizohusisha zaidi ya waj umbe 7,000 kutoka Nchi 182 Wanachama wa Umoja wa Mataifa. Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS, Stella Vuzo amekuwa akizungumza na washiriki mbalimbali kuhusu walivyonufaika na mkutano huo na hapa ni mmoja wao kutoka jamii za wafugaji ambao duniani kote mabadiliko ya tabianchi yanawaathiri moja kwa moja.

Sauti
2'14"