Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Tunatarajia kujadiliana na nchi mbali mbali ili kubadilishana mawazo:Waziri-Kariuki

Mkutano wa sitini wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake, CSW60 umeng’oa nanga makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano huo ulianza Machi 14 hna unaendelea adi Machi 24. Kauli mbiu ya mwaka huu imejikita katika kuwawezesha wanawake na uhusiano wake na malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs ambayo yameridhiwa mwaka jana.

Nchi wanachama kupitia wawakilishi wao wanashiriki mkutano ambao unachangia kwa kiasi kikubwa katika kubadilishana mawazo ili kuwezesha lengo la usawa wa kijinsia 50 kwa 50 kufikiwa mwaka 2030.

CSW yango'a nanga, mwelekeo na matarajio

Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani umeng'oa nanga hapo jana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Wadau mbali mbali kutoka sehemu mbali mbali wamehudhuria mkutano huo.  Maudhui ya mkutano mwaka huu ni kuangalia jinsi ya kuwawezesha wanawake sambamba na maendeleo endelevu SDG's.

Katika makala hii, Assumpta Massoi amekutana na washiriki wa mkutano huo kutoka Afrika Mashariki kuangalia ni mambo gani yanafanyika..

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani

Juma hili mnamo Machi nane dunia imeadhimisha siku ya wanawake ambapo haki, ustawi na hata changamoto za kundi hilo vimeangaziwa . Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni chukua  hatua, usawa wa kijinsia  katika utekelezaji wa malengo ya mendeleo endelevu SDGS kufikia 50 kwa 50.

Siku ya Wanawake yaadhimishwa na dhamira mpya na muziki kutoka Trinidad

Wiki hii, Jumanne Machi Nane, ilikuwa Siku ya Wanawake Duniani. Ikiadhimishwa kwa kauli mbiu: “Sayari ya 50 kwa 50 ifikapo mwaka 2030: Imarisha Juhudi za Kufikia Usawa wa Jinsia”.

Kilele cha maadhimisho ya siku hiyo, kilikuwa kwenye hafla iliyofanyika kwenye moja ya kumbi za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ikimulika jinsi ya kuongeza kasi na kuimarisha nguvu ya kutekeleza ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu.

VICOBA na mwelekeo wa kuwezesha #Planet5050

Lengo namba tano la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linaangazia usawa wa kijinsia. Hii inatokana na ukweli kwamba katika jamii, ukosefu wa usawa umesababisha madhila kwa wanawake licha ya ushiriki wao katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Nchini Tanzania harakati zinaendelea kukwamua wanawake na miongoni mwao ni kupitia baraza la uwezeshaji kiuchumi la Taifa, ambalo pamoja na mambo mengine linasaidia wanawake walio kwenye vikundi, mathalani VICOBA yaani benki za kijamii vijijini. Je wanasaidia vipi ili kusongesha harakati za Umoja wa mataifa?

UN Photo/B Wolff

Fursa za mafunzo zalenga kuwainua wanawake-Tanzania

Lengo la tano la malengo ya maendeleo endelevu au Ajenda 2030 linaangazia usawa wa kijinsia. Katika kufanikisha lengo hili mikakati muhimu inapaswa kuwekwa ili kuhakikisha kwamba nchi zinafanikiwa. Moja ya mikakati muhimu katika kufanikisha lengo ni kutoa mafunzo kwa wanawake n wanaume ambako nchini Tanzania baadhi ya wanawake wamepata mafunzo yanayolenga kuwainua kiuchumi. Benson Mwakalinga kutoka Redio Washirika Kyela FM ya Mbeya Tanzania amezungumza na baadhi yao, ungana naye katika makala hii.

Wanawake Kenya wajikwamua na umasikini

Kuelekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na ustawi wa wanawake UN Women, linadhihirisha miradi mbali mbali linaloendesha katika kukuza ustawi wa wa kundi hilo.

Mathalani nchini Kenya, UN Women kwa kushirikiana na Serikali ya nchi hiyo imeendesha mradi uliowezesha wanawake kiuchumi kama anavyosimulia Grace Kaneiya katika makala ifuatayo..

Nchini DRC, wanawake ni wengi kuliko wanaume, kwanini hawapewi nafasi sawa?

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, usawa wa kijinsia bado ni changamoto. Wanawake wanashikilia asilimia 9 tu ya viti vya bunge na chini ya asilimia 5 ya viti vya senate kwa mujibu wa Umoja wa Wabunge Dunaini, IPU. Kadhalika, vita viliyoikumba mashariki mwa nchi hiyo tangu mwaka 1996 vimesababisha mateso mengi hasa kwa wanawake ambao wamekuwa wahanga wa ubakaji na ukatili wa kingono uliotumiwa kama silaha ya vita.

Umoja wa wanawake unabadili maisha Guinea-Conakry

Kuelekea siku ya wanawake duniani tarehe Nane mwezi huu wa Machi, Umoja wa Mataifa unapigia chepuo ushirikishaji wa wanawake kwenye utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ukiangazia lengo namba Tano la usawa wa kijinsia.

Lengo hilo linagusia pamoja na  mambo mengine wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi katika ngazi mbali mbali.