Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

VICOBA na mwelekeo wa kuwezesha #Planet5050

VICOBA na mwelekeo wa kuwezesha #Planet5050

Pakua

Lengo namba tano la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linaangazia usawa wa kijinsia. Hii inatokana na ukweli kwamba katika jamii, ukosefu wa usawa umesababisha madhila kwa wanawake licha ya ushiriki wao katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Nchini Tanzania harakati zinaendelea kukwamua wanawake na miongoni mwao ni kupitia baraza la uwezeshaji kiuchumi la Taifa, ambalo pamoja na mambo mengine linasaidia wanawake walio kwenye vikundi, mathalani VICOBA yaani benki za kijamii vijijini. Je wanasaidia vipi ili kusongesha harakati za Umoja wa mataifa? Stella Vuzo amezungumza na Katibu Mtendaji wa baraza hilo Beng’I Issa kando mwa kongamano lililoandaliwa na UN Women kwa ushirikiano na ubalozi wa Sweden nchini Tanzania kuhusu uwezeshaji wanawake wajasiriamali. Hapa kwanza Ben’g’I anaelezea kuhusu VICOBA.

Photo Credit
VICOBA vyawezesha wanawake kuimarisha akiba na kushiriki shughuli za kiuchumi. (Picha:UNDP-Tanzania)