Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lugha ya mama kama chombo cha kutoa mafunzo Afrika Mashariki

Lugha ya mama kama chombo cha kutoa mafunzo Afrika Mashariki

Pakua

Februari 21 ni siku ya lugha ya mama duniani.Kauli mbiu ya mwaka huu ni:  “Elimu yenye ubora, lugha inayotumika kufundisha na matokeo yake.” Hii inasisitiza umuhimu wa lugha ya mama kwa ajili ya ubora wa elimu na katika uwepo wa lugha mbalimbali.

Katika ujumbe wake wa mwaka huu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO Irina Bokova amesema kwamba Lugha za mama katika muktadha wa lugha zaidi ya moja ni kiungo muhimu katika kuhakikisha elimu bora, ambayo  ni msingi wa kuwaimarisha wanawake na wanaume katika jamii.

UNESCO imesema kwamba ni muhimu kutambua na kuimarisha nguvu hii ili kutomuacha mtu yeyotenyuma kwa ajli ya mustakabhali endelevu kwa wote. Je hali ikoje Afrika Mashariki?

Photo Credit
@UNESCO