Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Maadhimisho ya muongo wa watu wenye asili ya afrika

Kwa zaidi ya miaka mia 400, biashara ya utumwa imekuwa janga lililoikumba Afrika, ikikadiriwa kwamba zaidi ya watu milioni 15, wanaume, watoto na wanawake wamekuwa wahanga wa biashara hii kupitia bahari ya Atlantiki.

Hadi leo, Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba watu wapatao milioni 200 wenye asili ya Afrika wanaishi Marekani na kwenye bara la Amerika na Karibia.

Wengi wao bado hukumbwa na unyanyapaa na ubaguzi, wakikosa fursa sawa za kielimu, kisiasa na kiuchumi.

Kongamano la WIPO lakutanisha wabunifu wa mitindo Afrika kuhusu hati miliki

Sekta ya ubunifu wa mitindo barani Afrika ina uwezo mkubwa wa kukua, kwani kuna wingi wa talanta na ubunifu kote barani. Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Hati Miliki Duniani, WIPO, matumizi yafaayo ya hati miliki yanaweza kuchangia maendeleo endelevu ya sekta hiyo. Kwa mantiki hiyo, hivi karibuni, WIPO iliandaa kongamano kuhusu hati miliki kwa bara la Afrika linaloibuka, mjini Dakar, Senegal, ambako pia kulifanyika maonyesho ya sanaa na mitindo, kama anavyosimulia Joshua Mmali katika Makala hii.

Afrika kujadili fursa za mkataba wa COP21: Muyungi

Mjumbe wa kamati ya wataalamu wa Afrika wanaowashauri marais kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, ambaye pia ni msimamizi wa mabadiliko ya tabianchi Tanzania ,Richard Muyungi amesema nchi za Afrika zitakutana kuangalia fursa zilizopo baada ya mkataba wa COP21.

Akihojiwa na Joseph Msami wa idhaa hii Bwana Muyungi amesema baada ya dunai kushuhudia makubaliano ya mkataba wa mabadiliko ya tabianchi mjini Paris, nchi za Afrika zinapaswa kutathimini hatua za kuchukua ili kunufaika.

Awali anaeleza bara hilo linakusudia kufanya nini kupitia mikutano ya wataalamu.

UN Photo - Jean-Marc Ferre

Mkuu mpya wa UNAMID awasili Darfur kuanza kazi rasmi:

Mkuu mpya wa vikosi vya pamoja vya Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika vya kulinda Amani Darfur UNAMID , Martin Uhomoibhi amewasili Darfur Sudan kuanza rasmi majukumu yake.

Bwana Uhomoibhi amesema , Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa wana nia njema kabisa ya kusaidia pande kinzani kawenye mgogoro wa Dafur kufikia suluhu kwa njia ya Amani.

Flora Nducha amezungumza na Jumbe Omari Jumbe Mkuu wa Radio UNAMID kuhusu matarajio na hamasa baada ya kuwasili mkuu huyo mpya wa UNAMID...

(MAHOJIANO DAFUR)

Huduma za afya kwa wazee Afrika Mashariki

Uzee hutizamwa na jamii kama kipindi kigumu kilichojawa na kadhia nyingi. Moja ya kadhia inayokumba kundi hili ni  upatikanaji wa huduma za kijamii mathalani afya.

Malengo mapya ya maendeleo endelevu SDGS yaliyoridhiwa na nchi wanachama hivi karibuni yanaanisha nafasi ya wazee katika kupatiwa huduma ya afya na kuangalia ustawi wao kwa ujumla. Lengo namba tatu lisemalo afya bora na ustawi pamoja na makundi mengine katika jamii linaangazia afya za wazee ambao mara nyingi husahaulika.

DR Congo yaorodhesha wakimbizi 6,000 toka Sudan Kusini:

Takribani wakimbizi 6000 wamewasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakitokea majimbo ya Equatoria Sudan Kusini.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR watu hao ambao pia wanajumuisha raia wa Congo wanaongia kwenye eneo la Dungu na walianza kukimbia mwezi Desemba kama anavyothibitisha, Teresa Orango afisa habari wa Kanda ya Afrika ya Mashariki na Kati wa UNHCR alipozungumza na Flora Nducha..

(MAHOJIANO TERESA ORANGO)

Bora baridi kuliko mashambulizi huko Syria; wasema wakimbizi

Mzozo wa Syria ukiwa umeingia mwaka wa tano, wakimbizi waliosaka hifadhi kwenye bonde la Bekaa nchini Lebanon wanahaha kujinusuru na baridi kali. Theluji ya kwanza imeanguka na maelfu ya wakimbizi ambao tayari wamekumbwa na machungu, wanazidi kuhaha, na miongoni mwao ni Abu Hamada.

Yeye, mkewe na watoto wao 10 waliwasili Bekaa miaka miwili iliyopita na sasa wanahaka kuhakikisha kuwa wanapata joto la kutosha ili kunusuru familia yao. Vifaa vya kutoa joto, mafuta na makazi ni usaidizi wa Umoja wa Mataifa na wadau wake wa misaada lakini bado hali si shwari.