Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

uhifadhi wa sauti na video Afrika Mashariki

Oktoba 27 ni siku ya kimataifa ya uhifadhi wa sauti na video.Siku hii ambayo ilipitishwa mwaka 2005 na BAraza Kuu la Umoja wa Mataifa inalenga kuchagiza uelewa wa hatua madhubuti za utunzaji wa nyaraka za sauti na video kama kiungo muhimu cha utambulisho wa kitaifa.

Katika ujumbe wa mwaka huu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO, Irina Bokova amesema kwamba kuna miaka 10 hadi 15 ya kubadilisha sauti za video zilizopo kutoka analojia kwenda dijitali ili kuhakikisha uhifadhi wake.

Ikiadhimisha miaka 70 ya UM, Sudan Kusini yakumbushwa kuhusu amani

Hisia na kumbukumbu za nchi kutumbukia katika machafuko ni miongoni mwa matukio yalioghubika maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa mjini Juba nchini Sudan Kusini.

Hizi ni sherehe zilizofanyika chini ya ulinzi wa askari walinda amani katika ofisi za ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo. Ungana na Jospeh Msami aliyemulika sherehe hizo katika makala ifutayo.

Wanawake hukumbwa na madhila wakisaka kipato

Harakati za kukomboa mwanamke kiuchumi na kijamii hukabiliana na changamoto kadhaa wakati wa mcahakato wa kusaka kipato kwa kundi hilo. Mathalani wanawake wanaofanya katika mazingira magumu hukumbana na changamoto za kiafya na nyinginezo.

Nchini Uganda wanawake wajasiriamali katika migodi ya chumvi wanakabiliwa na magumu hadi kaisi cha kutishia kuvunja ndoa zao. Ungana na John Kibego katika makala ifuatayo.

UN Photo/B Wolff

Harakati za kusaka maji na usawa wa kijinsia Tanzania

Upatikanaji wa maji safi na huduma za kujisafi ambalo ni lengo namba sita la mendeleo endelevu SDGS ni miongoni mwa mahitaji muhimu katika nchi zinazoendelea. Nchini Tanzania mkoani Mara uhaba wa maji unaripotiwa katika baadhi ya maeneo na kusababisha baadhi ya wakazi kupoteza muda mwingi kusaka maji. Lakini wakati adha hiyo ikiendelea nayo, huku ukame nao ukichochea tatizo hilo, wanaume nao wamechukua jukumu la kusaidia wanawake katika kusaka rasilimali hiyo adhimu katika kuboresha utendaji kazi majumbani.

Mradi wa Innovate Kenya waleta nuru kwa sekta ya teknohama

Katika kutambua umuhimu wa teknohama katika jamii mradi wa Innovate Kenya umeanzishwa nchini Kenya kwa lengo la kuchagiza uwekezaji katika teknolojia kupitia makundi ya vijana.

Uti wa mgongo wa mradi huu ni progamu ya mafunzo kupitia mtandao kuhusu uwekezaji wa kijamii inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi duniani UN-Habitat ambao wanatoa mafunzo. Kupata kwa undani ungana na Grace Kaneiya katika makala hii.

UNICEF na wadau waleta nuru kwa wazazi wenye VVU Tanzania

Lengo namba Tatu la malengo ya maendeleo endelevu. SDGs yaliyopitishwa hivi karibuni na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa linagusia ustawi wa afya kwa watu wote bila kujali umri, jinsia na hali yoyote aliyonayo.

Mwelekeo wa kufanikisha afya hiyo hata kwa watu wanaoishi an virusi vya Ukimwi unatia moyo kutokana na huduma zinazoendelea kutolewa kwa wajawazito wanaoishi na VVU.

Mtoto wa kike, sauti yake yapazwa

Watoto wa kike wanapaswa kupewa fursa wanayostahili ili wawe  viongozi, wafanyabiashara na raia wa siku za usoni, ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, wakati wa maaadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike Oktoba 11.

Kwenye ujumbe wake kwa siku hiyo Katibu Mkuu amesema ili kuwezesha watoto wa kike ni lazima kuwasaidia kuepukana na ndoa na mimba za utotoni, ukeketaji, na vile vile kuwapatia elimu bora na kuhakikisha wanakuwa na afya nzuri na ujuzi kuhusu haki zao katika maswala ya afya ya uzazi.

Hafla ya maadhimisho ya wiki ya Afrika yapambwa kwa nyimbo na vyakula

Wakati wiki ya Afrika ikitia nanga hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York kumefanyika mikutano ambayo imelenga kujadili maswala yanayolenga bara hilo. Kwani Afrika ni moja ya ajenda kuu ya Umoja huo.

Kwa mantiki hiyo kumefanyika hafla maalum ya kuadhimisha wiki hii Alhamisi mchana kwa malengo ya kuwaleta pamoja watu kutoka Afrika kujumuika pamoja.

Je ni yapi yaliyojiri? Grace Kaneiya alikuwa shuhuda wetu, basi ungana naye katika makala hii.

Mamilioni wanakabiliwa na uhaba wa chakula nchi zinazoendelea: WFP

Siku ya kimataifa ya chakula ikiadhimishwa mnamo Oktoba 15, ripoti za shirika la Umoja wa Mataifa la chakula WFP zinaonyesha kuwa mamailioni ya watu katika nchi zinazoendelea wana uahaba wa chakula.

Ungana na John Kibego katika makala ifutayo ambapo amekwenda katika soko nchini Uganda na kisha kumtembelea mama ambaye kwa mujibu wa utamaduni wa eneo hilo ana wajibu wa kuhudumia chakula kwa familia.