Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Maonyesho ya 'Saba Saba" Tanzania na jukwaa la wanawake la maendeleo!

Wanawake, kila uchao harakati za kukwamua kundi hilo zinazidi kuimarika sambamba na lengo namba Tatu la maendeleo ya milenia yanayofikia ukomo mwezi Septemba mwaka huu. Lengo hilo linasaka usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake. Uwezeshaji unaozungumziwa ni ule wa kuweka fursa za kisheria na kisera ambazo kwazo wanawake wanaweza kushiriki katika shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii bila vikwazo. Nchini Tanzania harakati za kumkwamua mwanamke zinaimarika na zimekuwa dhahiri katika maonyesho ya kimataifa ya biashara al maarufu Saba Saba yanayofanyika jijini Dar es salaam.

Shamrashamra za miaka 55 ya Uhuru wa Somalia

Somalia,  nchi ambayo imekuwa katika vita kwa zaidi ya miongo miwili sasa inaibuka kutoka katika majivu ya vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe. Changamoto bado zipo, iwe kisiasa, kiuchumi na kijamii lakini changamoto hizo hazikuzuia serikali  ya shirikisho na wananchi kusherehekea miaka 55 ya uhuru wa nchi hiyo. Sherehe zilifanyika maeneo mbali mbali ikiwemo  Baidoa, Beletweyne na Kismayo. Lakini katika makala hii, Assumpta Massoi anakupeleka Mogadishu, mji mkuu wa Somalia ambako ndiko sherehe za kitaifa zilifanyika na kuhudhuriwa na wananchi na wageni mbali mbali.

Siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya madawa ya kulevya

Juhudi za kukabiliana na madawa ya kulevya ni lazima ziambatane na kazi zetu za kuchagiza fursa kupitia maendeleo sawa na endelevu. Ni lazima tuendelea kujaribu kuwafanya wanyonge na wadhaifu wawe na nguvu. Huo ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wa siku ya kupinga matumizi ya madawa ya kulevya inayoadhimishwa Juni 26 kila mwaka.

Siku hii imekuwa ikiadhimishwa tangu kupitishwa na  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Disemba 1987 kama sehemu ya juhudi za ulimwengu kuchagiza vitendo na ushirikiano ili kushinda vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya.

Ufugaji nyuki wakwamua maisha ya wafugaji Uganda

Ili kukabiliana na umasikini ambalo ni lengo la kwanza la malengo ya maendeleo ya  milenia linalofikia ukomo mwaka huu ufugaji wa nyuki ni moja ya mbinu ya kujiongezea kipato ambayo imeonesha mafaniko nchini Uganda.

John Kibego kutoka Hoima nchini humo anaangazia namna ufugaji wa nyuki ulivyobadili maisha ya wafugaji na jamii husika.