Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Wakimbizi wa Syria waendelea kumiminika Lebanon

Dunia hivi sasa inaelekeza macho yake nchini Syria nchi ambayo mzozo unaoendelea umesababisha madhila kwa raia wa nchi hiyo ikiwamo kuwa wakimbizi. Raia wa nchi hiyo wamejikuta wakimbizi katika nchi za jirani mathalani Iraq, Uturuki na kwingineko.

Lakini hali ni mbaya zaidi nchini Lebanon ambapo lundo la wakimbizi wako nchini humo. Ungana basi na Grace Kaneiya anayeangazia adha za wakimbizi wa Syria walioko nchini Lebanon.

Michezo yatumika kupinga ulemavu Bosnia

 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, kwa kushirikiana na washirika wanafanya kampeni maalum ya kupambana na ulemavu kwa watoto kwa kutumia michezo ili kuifikia jamii.

 Kampeni hii inayowahusisha watoto inalenga kubadilisha mtizamo wa jamii kuhusu watoto wanaosihi na ulemavu ili kuwajumuisha katika kila nyanja kwenye jamii.

 

 

Wakimbizi wa Syria walioko Lebanon wapatiwa hifadhi Ujerumani

Wakati mapigano nchini Syria yakizidi kupamba moto Serikali ya Ujerumani imekubali kuwapatia ukazi wa muda raia elfu tano wa Syria wanaoishi Lebanon, na hiyo ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM.

Patrick Maigua amefanya mahojaino na Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe kufahamu undani wa mchakato wa kuwapeleka wakimbizi hao wa Syria nchini Ujerumani.