Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

03 AGOSTI 2022

Hii leo jaridani tunamulika:
1.    Kuruhusiwa kwa meli ya kwanza yenye shehena ya nafaka kutoka Ukraine kuelekea Lebanon tayari kuuzwa kwenye soko la kimataifa. 
2.    Wanufaika wa Chuo cha Mafunzo ya kutengeneza ndege zisizo na rubani, (drones) huko Malawi watoa shukrani kwa Umoja wa Mataifa, kulikoni?
3.    Makala tunakwenda DRC ambako ni simulizi tamu na chungu miongoni mwa wakimbizi wa ndani na wakimbizi kutoka nje ya nchi kutokana na  ukata unaokabili UNHCR

Sauti
11'24"

02 AGOSTI 2022

Hii leo kwenye jarida likiletwa kwako na Assumpta Massoi:Habari kwa Ufupi: Uzinduzi wa ubia wa kimataifa kuhakikisha watoto wachanga wanapata matibabu dhidi ya Virusi vya Ukimwi, kisha UNHCR huko DRC inaweza kusitisha mgao wa kimkakati kwa wakimbizi kutokana na ukata na hatimaye ni WHO yazindua ombi la takribani dola milioni 124 kusaidia changamoto za njaa na afya kwenye pembe ya Afrika. Mashinani tunabisha hodi Yemen kwenye kambi ya wakimbizi ambayo hali yake ni taaban. Karibu!

 

Sauti
12'41"

01 AGOSTI 2022

Hii leo jaridani tunaanzia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako kumefanyika tukio la kuaga walinda amani watano wa Umoja wa Mataifa waliouawa wakati wa maandamano na uvamivi wa vituo vya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO huko Butembo na Goma jimboni Kivu Kaskazini. Tunamulika pia kuanza kwa wiki ya unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama ambayo imeanza rasmi leo.

Sauti
12'40"