Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

01 AGOSTI 2022

01 AGOSTI 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunaanzia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako kumefanyika tukio la kuaga walinda amani watano wa Umoja wa Mataifa waliouawa wakati wa maandamano na uvamivi wa vituo vya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO huko Butembo na Goma jimboni Kivu Kaskazini. Tunamulika pia kuanza kwa wiki ya unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama ambayo imeanza rasmi leo. Makala tunakwenda Dakawa mkoani Morogoro nchini Tanzania kumulika Bonanza la kuelimisha jamii kuhusu haki na ulinzi wa mtoto na mashinani ni makubaliano ya kihistoria ya kuanza kutengeneza kwa bei nafuu kinga dhidi ya VVU kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Audio Duration
12'40"