Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

02 MACHI 2022

Katika jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Leah Mushi anakuletea

-Idadi ya watu waliokimbia mashambulizi nchini Ukraine katika kipindi cha siku 6 zilizopita ni zaidi ya 870,000, limesema hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, kupitia jukwaa lake lililozindua ili kuonesha takwimu za watu wanaokimbia wakiwemo raia na wageni. 

Sauti
11'29"

01 Machi 2022

Karibu kusikiliza jarida ambapo miongoni mwa utakayosikia ni pamoja na ombi la fedha za kusaidia wakimbizi nchini Ukraine

Hali inavyoendelea nchini Madagascar baada ya kukumbwa na vimbunga vinne katika kipindi kifupi 

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa Tanzania kikosi cha TANZBAT-8 wametoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC

Na FAO imehimiza wavuvi wadogo wafdogo wasipuuzwe kwakuwa wanaumuhimu mkubwa hasa kwenye masuala ya lishe. 

Sauti
15'11"