Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

02 MACHI 2022

02 MACHI 2022

Pakua

Katika jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Leah Mushi anakuletea

-Idadi ya watu waliokimbia mashambulizi nchini Ukraine katika kipindi cha siku 6 zilizopita ni zaidi ya 870,000, limesema hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, kupitia jukwaa lake lililozindua ili kuonesha takwimu za watu wanaokimbia wakiwemo raia na wageni. 

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema ingawa nchi nyingi duniani zimejumuisha wakimbizi katika mipango yao ya utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19, bado wakimbizi wengi wanashindwa kupata chanjo hiyo kutokana na vikwazo mbalimbali ikiwemo kukosa nyaraka za kujisajili kupata chanjo hiyo.

-Kundi ongozi la kimataifa katika kukabili usugu wa viuavijiumbe maradhi hii leo limetoa wito kwa nchi zote duniani kupunguza taka za viuavijiumbe maradhi zinazotupwa hovyo na kuharibu mazingira kwa kutaka kufanyika utafiti zaidi na kuchukua hatua za kutupa kwa uangalifu taka hizo za dawa kutoka kwenye vyakula na mifumo ya afya ya binadamu, Wanyama pamoja na viwandani

-Mada yetu kwa kina leo  leo ni siku ya pili ya mkutano wa wakuu serikali na nchi zenye bahari kujadili masuala ya uvuvi , wavuvi nchini Tanzania wamezungumza. Wanasema nini?

-Na mashinani utamsikia Balozi mwema wa UNICEF James Elder akiwa mpakani mwa Ukraine na Moldova akitathimini hali ya wakimbizi wanaokimbia vita Ukraine

Audio Credit
UN News/ Leah Mushi
Audio Duration
11'29"