Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

Jarida 02 Februari 2022

Miongoni mwa tuliyonano kutoka UN


Leo ni mara ya kwanza kuadhimishwa kwa siku ya kimataifa ya maeneo oevu  tangu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lipitishe azimio mwezi Agosti mwaka jana 2021. Tunabisha hodi nchini Laos kuona harakati za kuhifadhi maeneo hayo adhimu.


Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF limelaani vikali mauaji ya watoto 15 katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Sauti
11'14"

Jarida 01 Februari 2022

Miongoni mwa tuliyonayo hii leo kutoka Umoja wa Mataifa 

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO limetoa ripoti mpya inayoonesha kuwa mifumo ya usimamizi wa taka za afya duniani kote hivi sasa imezidiwa uwezo kutokana na maelfu ya tani za taka zinazotokana na vifaa vilivyotengenezwa kwa ajili ya kukabiliana na janga la COVID-19 na hivyo kutishia afya ya binadamu na mazingira na wakati huo huo kufichua hitaji kubwa la kuboresha udhibiti wa taka zinazozalishwa kutokana na huduma ya tiba. 

Sauti
13'3"