02 Machi 2021
Hii leo jaridani, Flora Nducha anaanzia huko Somaliland ambako Umoja wa Mataifa umepeleka mashine za kuwezesha wagonjwa kuvuta hewa ya oksijeni wakati huu hospitali zimezidiwa kutokana na janga la COVID-19 linaloleta mkwamo kwa wagonjwa kupumua. Kisha anammulika Mkurugenzi Mkuu mpya wa shirika la biashara duniani, WTO, Ngozi Okonjo-Iweala ambaye amenaza rasmi jukumu lake akiwa mwanamke wa kwanza na pia mwafrika wa kwanza kushika wadhifa huo.