Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UNICEF/Jame Ekwam

Mafuriko Kenya: UNICEF yapatia wakazi wa Kaunti ya Mto Tana fedha za kujikimu

Mvua za El-nino zikiendelea kutikisa ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo taifa la Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo kwa ufadhili wa serikali ya Uingereza limepatia msaada wa hali na mali wakazi wa kaunti ya mto Tana walioathiriwa na mafuriko hayo.  Cecily Kariuki na taarifa zaidi.

Video ya UNICEF Kenya inaanza ikimuonesha mkazi huyu wa hapa mji wa Garseni katika kaunti ya mto Tana akiwa amebeba kikapu huku akiwa na watoto wake wawili wakirejea nyumbani.

Sauti
2'6"
© UNOCHA/Ayub Ahmed

Umoja wa Mataifa umeanza kufikisha misaada kwa wakimbizi ili kujiandaa na mafuriko

Tukiwa katika msimu wa mvua kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, tuelekee nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA limesema wao na wadau wao wamejiandaa kufikisha mahitaji kwa watu 770,000 katika wilaya 22 za nchi hiyo ambao wanatarajiwa kuathirika na mvua za msimu huku wakieleza kuwa wakimbizi wa ndani wanatarajiwa kuaahirika ziadi.

Sauti
2'17"
UNDP Somalia/Fadhaye

Somalia: Bilan yadhihirisha kuwa wanawake wanahabari wanaweza kufanya kazi pamoja na kwa uthabiti

Leo ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mwaka huu ikibeba maudhui “Vyombo vya Habari kwa ajili ya Sayari: Uandishi wa habari katika kukabiliana na mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi”  kwani Umoja wa Mataifa unasema mchango wa wanahabari na vyombo vya habari ni kiini katika kuhabarisha na kuelimisha umma kuhusu changamoto hiyo ya tabianchi. 

Audio Duration
2'23"
UN News/Ziad Taleb

UN: Wananchi wa Gaza wako katika jakamoyo wakisubiri taarifa kuhusu wito wa kusitisha mapigano

Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za kuaminika za usambazaji wa misaada kwa watu wanaohitaji kwa udi na uvumba zinapatikana. 

Sauti
1'57"
© WHO

UNRWA: Watoto 17,000 wametenganishwa na wazazi au familia zao Gaza

Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya hii leo juu ya idadi kubwa ya watoto ambao wako peke yao Gaza, ama wamepoteza wazazo au kutenganishwa nao pamoja na jamaa wa familia wakati huu ambapo hawawezi kuhudhuria masomo na shule nyingi zikigeuka kuwa makazi ya wakimbizi wa ndni. 

Kwa mujibu wa tarifa fupi ya UNRWA iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa X, shirika hilo linasema maisha ya watoto Gaza yamekuwa jinamizi na takriban 17,000 wako peke yao hawana wazazi au walezi ama wametenganishwa na familia zao.

Sauti
1'59"
© WFP/Michael Tewelde

Wananchi nchini Ethiopia wapongeza mfumo mpya wa kutambua wenye uhitaji

Nchini Ethiopia Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP na wadau wake waanafanya kazi kwa kushirikiana na jamii kutambua wale wenye uhitaji zaidi wa msaada wa kibinadamu, na wananchi wamepongeza WFP kwa mfumo huu mpya wa kutambua wenye uhitaji zaidi 

Ethiopia ni moja ya nchi zinazoendelea kukabiliana na athari za mizozo mingi inayoingiliana kama vile ukame, mafuriko pamoja na mizozo. Ili kukabiliana na mahitaji yanayokua WFP na wadau wake wameamua kuanzisha mfumo mpya wa kutambua familia zenye uhitaji zaidi miongoni mwa wanajamii. 

Sauti
2'28"
© UNICEF/UNI492302/Mohamdeen

Raia Sudan wakumbwa na kihoro kufuatia mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF

Huko nchini Sudan jimboni Darfur Kaskazini, hususan mjini El-Fasher na viunga vyake mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa RSF yanazidi kuwa na madhara kwa rai ana kumtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk. Katika kufahamu hali iko vipi, Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Seif Magango msemaji wa ofisi ya Kamishna Türk kutoka Nairobi, Kenya na anaanza kwa kueleza nini hasa kinamtia hofu Kamishna huyo.

Sauti
2'11"
©UNHCR/Ruben Salgado Escudero

Simulizi ya mwanamke aliyebakwa na kupata ujauzito wakati wa mzozo Sudan

Mwaka mmoja wa mzozo nchini Sudan umewafanya wananchi wengi kukimbia maeneo waliyokuwa wakiishi kusaka hifadhi pamoja na kukimbilia nje ya nchi. Pamoja ya kukimbia vita lakini pia wanasalia na majeraha ndani ya mioyo yao kutokana na masahibu waliyopitia. Mmoja wao ni Bi. Fatima ambaye alibakwa na kupata ujauzito. 

Fatima sio jina lake halisi, tunalitumia hili ili kuficha utambulisho wake na hapa anaanza kueleza yale yaliyomsibu akiwa mikononi mwa wanamgambo wenye silaha.

Sauti
2'2"