Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UNICEF/Sebastian Rich

Wawanufaisha Wanawake na watoto Malawi wanufaika na mradi wa kukuza lishe (SUN)

Mradi wa  ushirikiano kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na Seriali ya Malawi kuboresha hali ya lishe ya wanawake wajawazito, akina mama na watoto wenye umri chini ya miaka mitano umekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi nchini Malawi. Taarifa inasomwa na Hilda Phoya.

Mradi wa kuboresha hali ya lishe ili kupambana na utapiamlo katika wilaya sita za nchini Malawi, ni msaada mkubwa wa kidunia ambao unazileta pamoja nchi kadhaa katika juhudi za kuweka sera za nchi katika kutekeleza mipango yenye malengo ya pamoja kuhusu lishe.  

Sauti
2'55"
UN Development Programme

India, mradi wa IFAD wawanawirisha wanawake wa vijijini

Kutana na wanawake wa Tejaswini nchini India,  ikimaanisha kwamba ni wanawake walionawiri na kuwezeshwa. Kupitia mradi wa kuwapa mafunzo wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD wameweza kujitegemea, kusaidia familia zao , kusaidia na kushamiri. Taarifa inasomwa na Jason Nyakundi.

Katika jimbo la Marastra nchini India wanawake hawa walionawiri au Tejaswini ni sehemu ya wanawake milioni moja wa India walio katika program ya uwezeshaji wanawake vijijini inayofadhiliwa na IFAD.

Sauti
2'38"
VIDEO YA UNHCR

Uganda yafungua mpaka kwa muda kuruhusu wakimbizi kutoka licha ya COVID-19

Hatimaye Uganda imeruhusu raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC waliokimbia mapigano nchini mwao wapatiwe hifadhi baada ya kushindwa kuingia nchini humo tangu mwezi Mei mwaka huu kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. Taarifa inasomwa na John Kibego

Uganda imefunga mipaka yake ya nje na pia imepitisha hatua za kuepusha kuchangamana ndani ya taifa hilo ambalo hadi sasa limeripoti kuwa na wagonjwa 889 na hakuna hata mmoja aliyefariki dunia.

Audio Duration
2'42"
IFAD

Wakuchi wa Afghanistan wasaidiwa na michoro na picha kuelewa jinsi ya kujikinga na Corona

Nchini Afghanistan,  hatua za kuzuia watu kuchangamana kwa lengo la kuepusha kusambaa kwa ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19, zimesababisha watu wapatao milioni 1.5 nchini humo kukabiliwa na njaa na ugumu wa maisha. Taarifa inasomwa na Assumpta Massoi.

Miongoni mwao ni wafugaji wa kuhamahama wa jamii ya wakuchi ambao kwa miezi mitatu iiyopita, wamesalia na kipato kidogo na kiasi kidogo cha chakula.

Sauti
2'21"
UNMISS\Nektarios Markogiannis

Zimamoto mjini Juba Sudan Kusini waishukuru UNMISS

Mamlaka mjini Juba Sudan Kusini zimeushukuru Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS ambao umetoa msaada wa magari mawili makubwa ya huduma za uzimaji moto katika nchi hiyo ambayo miundombinu yake na huduma za kijamii vimeharibiwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu kwa takribani miaka mitano. Taarifa inasomwa na Loise Wairimu.

Sauti
2'57"
IOM

IOM imesema Mashirikisho na jumuiya 200 kwa waathirika wa COVID-19 wanaobaguliwa

Viongozi wa jumuiya za ughaibuni na mashirika ya kijamii kutoka kote duniani wamekuja pamoja kutuma ujumbe ulio bayana  na wa mshikamano na watu wanaokabiliwa na vitendo vya chuki dhidi ya wageni, ubaguzi na hata ukatili kutokana na janga la corona au COVID-19 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM. Taarifa inasomwa na Jason Nyakundi.

Sauti
1'58"