Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Ubunifu wa nguo za magome ya miti na uhifadhi wa mazingira Burundi-Sehemu ya II

Katika  Juhudi za kuunda ajira na  kuhifadhi mazingira, msichana kutoka Burundi Annick Kabatesi ameanzisha mradi wa kutengeneza nguo zitokanazo na magome ya miti.  Nguo hizo zimetajwa kuwa zinazingatia uhifadhi wa mazingira. Bi. Kabatesi ambaye ni mwanamitindo pia amejijengea umaarufu mkubwa kwa  kutengeneza nguo hizo za magome ya miti  baada ya nguo hizo kuwavutia viongozi wakuu Serikalini.

Zeid kuanza ziara El Salvador tarehe 15 mwezi huu

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid zaRa'ad Al Hussein  atatembelea El Salvador kwa mwaliko wa serikali kuanzia tarehe 15 hadi 16 mwezi huu ili kujadili maendeleo na changamoto zinazohusu haki za binadamu nchini humo.

Bwana Zeid ambaye atakuwa Kamishna Mkuu wa kwanza wa haki za binadamu kutembelea El Salvador, atakutana na Rais Salvador Sánchez Cerén.

UN Photo/John Isaac

UM uko tayari kusaidia waathirika wa tetemeko Iran-Iraq

Umoja wa Mataifa uko tayari kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Jumapili jioni mpakani mwa Iran na Iraq na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa endapo utahitajika kufanya hivyo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, akiongeza kuwa ameshtushwa na athari zake, huku akitoa pole kwa familia za waathirika na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi.

Msaada kutoka kwa papa Francis kusaidia familia Sudan Kusini

Familia zinazokabiliwa na njaa nchini Sudan Kusini zitaweza kuhimili hali hiyo kufuatia msaada wa vikasha vya mboga  vilivyotolewa na kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis wakati huu ambapo uhakika wa chakula unatarajiwa kuwa mashakani zaidi miezi michache ijayo.

Zaidi ya watu elfu 30 huko Yei, jimbo la Equatoria kati watanufaika kutokana msaada huo wa Euro 25,000 zilizotolewa na Papa Francis kwa shirika la chakula na kilimo duniani FAO.

Huduma za kibinadamu ziruhusiwe bila vikwazo Ghouta:WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema watu wapatao 400,000 wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na afya na usalama katika eneo la Ghouta Mashariki mwa Damascus mji mkuu wa Syria.

WHO imesema katika eneo hilo watu  240 wanahitaji huduma ya dharura ikibidi kuhamishwa haraka kwa ajili ya matibabu.

Bi Elizabeth Hoff, ambaye ni  mwakilishi wa WHO nchini Syria anasema kwa miezi kadhaa, watu mashariki mwa Ghouta wamekuwa wakikosa huduma ya kibinadamu sababu kubwa ikiwa ni vikwazo katika eneo hilo ili kuwafikia walengwa.

IOM yasaidia wakimbizi kurejea nyumbani CAR

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM limekamilisha shughuli ya kuhamisha wakimbizi wa ndani 698 kutoka kambi ya muda karibu na kituo cha ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR, MINUSCA waliochukua hifadhi kufuatia mashambulizi ya 2016 mji wa Kaga Bandoro.

Zaidi ya wakimbizi 20,000 kutoka CAR waliwasili karibu na kituo hicho baada ya kikundi cha wapiganaji wa zamani wa Seleka kushambulia kambi ya wakimbizi wa ndani ya Evêché.

Utamaduni na burudani vyang’aa mkutano COP23

Mkutano wa 23 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP23 umefanyika wiki hii huko Bonn, Ujerumani, lengo kuu ni kuchagiza mbinu za kukabili mabadiliko ya tabianchi ambayo yanaendelea kuwa mwiba kwa wakazi wengi duniani. Kando na vikao kumefanyika pia burudani,basi ungana na Grace Kaneiya katika Makala ifuatayo

Ibara kwa Ibara- Tamko la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa

Kila mtu anastahili kuwa na haki zote na uhuru wote ambao umeelezwa katika tamko hili bila ubaguzi wa aina yoyote kama vile rangi, taifa, jinsia, lugha, dini, siasa, fikra, asili ya taifa la mtu, miliki , kuzailiwa au kwa hali nyingine yoyote.

Halikadhalika hakuna ubaguzi utakaotendwa kwa misingi ya kisiasa, kimamlaka au hadhi ya kimataifa ya nchi au utawala ambao mtu fulani anatoka, iwe ni huru, iwe chini ya  udhamini, isiyojitawala au chini ya mazingira mengine yenye udhibiti wa kimamlaka.

Sauti
52"

UNICEF na WHO kutoa chanjo dhidi ya surua huko Bangladesh

Ongezeko la hofu ya kuwepo kwa wagonjwa wa surura miongoni mwa wakimbizi wapya wa Rohingya waliowasili hivi karibuni nchini Bangladesh, imesababisha mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la kuhudumia watoto, UNICEF na lile la afya, WHO pamoja na serikali ya Bangladesh kuimarisha jitihada za chanjo dhidi ya ugonjwa huo kwenye kambi   za wakimbizi.

UNICEF imesema karibu watoto 360 000 wenye  umri kati ya  miezi sita hadi miaka 15 kwenye eneo la Cox’s Bazar nchini Bangladesh watapatiwa chanjo na pia katika mipaka yote ya kuingia Bangladesh.