Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawaziri wa ulinzi kutoka nchi 80 wanakutana kutathimini operesheni za ulinzi wa amani: UM

Mawaziri wa ulinzi kutoka nchi 80 wanakutana kutathimini operesheni za ulinzi wa amani: UM

Pakua

Wawakilishi na mawaziri wa ulinzi kutoka takribani nchi 80 duniani wanakutana kuanzia leo mjini Vancouver Canada ili kutathimini masula ya operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.

Akizungumzia umuhimu wa mkutano huo Atul Khare msaidizi wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya msaada mashinani amesema

(KHARE-1)

“Mkutano huu ni muhimu sana kwa sababu huu ndio wakati pekee wa kuzungumza na mawaziri wa ulinzi wan chi ambazo zinatupa walinzi wa amani 125, 000 ambao ni muhimu kwa kazi zetu. Pia mkutano huu utatupa fursa ya kuainisha mahitaji yaliyopo na yanayoendelea ya operesheni za amani.”

Ameongeza kuwa operesheni hizo za Umoja wa Mataifa hivi sasa zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa vifaa, wafanyakazi, huduma  zikiwemo madawa na hata walinda amani wanawake hivyo

(KHARE 2)

“Tuna tumai mapengo haya yatashughulikiwa na mawaziri hawa wakati wa majadiliano yetu mjini Vancouver na natumai kutakuwa na msukumo mkubwa kuhusu walinda amani wanawake katika mkutano huu.”

Photo Credit
UN Photo/Loey Felipe